Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-03 21:06:03    
Kobe-Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa lasihi kuzingatia watoto walioathirika na ukimwi

cri

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa na jumuiya nyingine tarehe 3 kwenye mkutano wa 7 wa sehemu za Asia na Pasifiki kuhusu ukimwi zilisihi kuwa ni lazima watoto wa sehemu hizo walioathirika na ukimwi wazingatiwe.

Ripoti iliyotolewa na jumuiya hizo inaonesha kuwa, idadi ya watoto yatima wa sehemu hizo, ambao wazazi wao walikufa kutokana na ukimwi, imefikia milioni 1.5, hivyo wanahitaji misaada. Aidha, watoto laki moja na elfu 21 wa sehemu hizo wameambukizwa virusi vya ukimwi au kuwa wagonjwa wa ukimwi.

Ripoti hiyo pia inazisihi nchi na sehemu husika zichukue hatua halisi, ili kuwalinda na kuwasaidia watoto hao, na kuwazingatia sana watoto walioambukizwa na virusi vya ukimwi pamoja na familia zao.

Mtendaji mkuu wa Shirika la mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa Bw. Peter Piot tarehe 2 huko Kobe alisema kuwa, hivi sasa sehemu ya Asia na Pasifiki iko kwenye kipindi ambapo ugonjwa wa ukimwi unalipuka mara kwa mara, hivyo nchi mbalimbali za sehemu hiyo zinapaswa kuchukua hatua halisi ili kuzuia ugonjwa huo usienee.

Takwimu mpya kabisa zimeonesha kuwa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi kwenye sehemu ya Asia na Pasifiki imepita milioni 8.