Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-04 16:41:51    
Kutumia likizo kwa kupanda meli kwenye Mto Changjiang

cri

Hivi sasa watalii wengi kutoka nchi za nje wanapenda kuja China katika majira ya siku za joto na kutumia likizo zao kwa kupanda meli kwenye Mto Changjiang, ambapo wanaweza kuchagua njia mbalimbali kwenda sehemu mbalimbali za eneo la Mto Changjiang kuangalia mandhari nzuri ya kando za mto. Bwana Huang Jie wa idara ya mawasiliano ya Shirika la utalii wa kimataifa la China akijulisha alisema:

Njia fupi ya utalii kwenye Mto Changjiang ni kufunga safari kutoka Chongqing hadi Yinchang, kwa kawaida mashirika ya utalii huwapangia watalii njia hiyo yenye vivutio vingi vya mandhari nzuri .

Wakifunga safari kutoka Chongqing kutembelea Mto Changjiang, watalii ni kama wanaingia kwenye njia moja yenye vivutio vya mandhari nzuri ya mto na milima. Kwenye njia hiyo wanaweza kuona Magenge matatu maarufu duniani, ambayo ni jina la jumla la bonde la magenge matatu ya Qutangxia, Wuxia na Xilingxia. Urefu wa bonde hilo ni kilomita 200 hivi, kijiografia sehemu hiyo ya milima mirefu ina vipengele vingi na utatanishi, mandhari yake nzuri ni ya ajabu, na pia kuna mabaki mengi ya kale huko. Mwalimu wa shule ya sekondari Bwana Wang Yang mara kwa mara aliwaongoza wanafunzi wake kufanya utalii kwenye sehemu hiyo alisema:

Nimekwenda sehemu hiyo mara kwa mara, hata nafahamu kila kitu cha sehemu hiyo, genge la kwanza Qutangxia ni genge fupi kuliko mengine mawili, na miamba ya kando zake mbili ni mirefu, ambapo kuna mabaki ya kale ya kuta zenye maandiko yaliyoandikwa na watu wa enzi mbalimbali za zama za kale za China, na chemchem ya phoenix; na kando mbili za genge la Wuxia kuna vilele 12 vya Mlima Wu, miongoni mwa vilele hivyo, kilele cha malaika kinapendeza na kujulikana zaidi, kilele hicho ni alama ya Mlima Wu; na genge la Xilingxia ni gende refu kuliko magenge mengine mawili, ambalo lina vipengelea mbalimbali vya hatari, kweli Magenge matatu ya Mto Changjiang yana vivutio mbalimbali vya kuwapendeza watu.

Hivi sasa mbali na kufanya utalii kwenye magenge matatu, watalii pia wanaweza kutembelea "magenge matatu madogo" ambayo yanaegemeana na genge la Wuxia kwenye Mto Ning, ambao ni tawi la mtiririko wa Mto Changjiang, magenge hayo matatu madogo yanaundwa na mabonde kadha wa kadha kama vile Bonde la Longmen lenye miamba mirefu na vilima virefu vinavyokabiliana, maumbo yake ni kama mlango mmoja mmoja mkubwa wa chuma. Wakipita bonde la Longmen watafika kando ya mto yenye utatanishi wa hatari, na wataingia kwenye Bonde la Tiguan?ambapo kando mbili za bonde hilo kuna mawe mengi yenye maumbo ya ajabu yaliyo kama michongo mingi ya maumbile inayopendeza, na katika Genge la Dichui la mbele kuna mawe mengi yenye maumbo mbalimbali yanayoloana na maji, hivyo miti na majani ya bondeni inaonekana ni ya kijani zaidi . Mtalii Dada Li Qing aliyefika huko alisema alijisikia kama amefika katika dunia inayosimuliwa kwenye hadithi. Alisema:

Kabla ya kufika kwenye "magenge matatu madogo" niliambiwa kuwa, magenge hayo madogo siyo yale magenge matatu maarufu, lakini ni yenye mandhari nzuri zaidi kuliko magenge matatu maarufu, nilipofika huko kweli niliona mandhari nzuri ya ajabu ya sehemu hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-03