Mkutano wa siku mbili wa baraza la uwekezaji la Asia ya mashariki, ulifungwa jana huko mji wa Weihai, ulioko katika sehemu ya mashariki ya China. Habari zinasema kuwa hivi sasa China imekuwa nguvu muhimu inayohimiza maendeleo ya uchumi wa Asia ya mashariki na inafanya kazi muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa uchumi wa sehemu hiyo.
Kauli-mbiu ya mkutano huo ni "Kufanya ushirikiano wa uwekezaji kuwa injini mpya ya ongezeko la uchumi wa Asia ya mashariki". Maofisa wa serikali, wanaviwanda na wataalamu zaidi ya 300 kutoka nchi 10 za China, Japan, Korea ya kusini ma Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki walikuwa na majadiliano kuhusu maendeleo ya uchumi, mazingira ya uwekezaji na ushirikiano wa mambo ya fedha ya sehemu hiyo.
Kwenye mkutano huo, umuhimu wa China katika maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo ulifuatiliwa na washiriki. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2004, jumla ya thamani ya biashara kati ya China na nchi nyingine 12 za Asia ilizidi dola za kimarekani bilioni 370 ikichukua theluthi moja ya jumla ya thamani ya biashara ya nje ya China katika mwaka huo. Naibu spika wa bunge la umma la China Bibi Gu Xiulian wa China alisema kuwa, maendeleo ya kasi ya uchumi wa China yamenufaisha nchi za Asia ya mashariki, alisema, "Uhusiano wa kishirikiano kati ya China na nchi za Asia ya mashariki ulikuzwa haraka, hususan ni kuwa karibu nchi zote za Asia ya mashariki zinaisafirishia China bidhaa nyingi zaidi kuliko bidhaa zinazoagiza kutoka China. Hali hiyo inaonesha kuwa China imetoa soko kubwa kwa nchi za Asia ya mashariki, na China imekuwa injini ya maendeleo ya uchumi ya Asia ya mashariki."
Kutokana na kuweko kwa soko kubwa na mustakabali mzuri wa maendeleo ya uchumi wa China, katika miaka ya karibuni viwanda na kampuni nyingi za nchi za Asia ya mashariki zilikwenda kuwekeza na kujenga viwanda nchini China. Hivi sasa nchi wawekezaji muhimu nchini China ni kutoka Asia ya mashariki. Takwimu mpya inaonesha kuwa katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu, mitaji ya kigeni iliyotumiwa na China ilizidi dola za kimarekani bilioni 22, ambazo karibu 30% zilitoka nchi za Asia ya mashariki. Miongoni mwa nchi za Asia ya mashariki, Japan ni nchi ya kwanza kwa wingi wa uwekezaji nchini China. Mratibu mkuu wa jumuiya ya uhimizaji wa biashara ya kimataifa ya Japan Bw. Nakata Yosio alisema kuwa hivi sasa viwanda na kampuni za Japan zilizowekeza nchini China zimezidi elfu 18 na mitaji iliyowekezwa nazo imefikia dola za kimarekani bilioni 48. Hapo zamani viwanda vya Japan vilipenda kuwekeza kwenye sehemu ya pwani ya mashariki ya China, lakini hivi sasa hali hiyo imebadilika, alisema, "Hivi sasa kuna viwanda vingi vya Japan vinavutiwa na sera mpya za China za 'Kustawisha sehemu ya magharibi' na 'Kustawisha kituo cha zamani cha viwanda cha kaskazini mashariki', na viko tayari kuingia sehemu hizo."
Inakisiwa kuwa ifikapo mwaka 2010, eneo la biashara huria kati ya China na umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki litaendelezwa kuwa eneo la biashara huria lenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1.7 na lenye thamani ya uchumi ya dola za kimarekani trilioni 2.4. Habari zinasema kuwa licha ya ujenzi wa eneo la biashara ya huria kati ya China na umoja huo, hivi sasa ujenzi wa eneo la biashara huria kati ya China na Korea ya Kusini pia umewekwa katika ratiba ya mazungumzo ya serikali za nchi hizo mbili.
Idhaa ya Kiswahili
|