Karidi siku ya Israel kuondoka kutoka eneo la Gaza inavyokaribia, ndivyo upinzani kutoka nguvu za kulia za Israel unavyozidi kuwa mkali siku hadi siku. Rais Moshe Katsav wa Israel tarehe 4 alionya kuwa, baadhi ya watu wenye msimamo wa kulia wanaochochewa huenda watamwua waziri mkuu wa Israel Bw. Ariel Sharon. Hivi sasa idara ya ulinzi ya Israel imeimarisha kazi ya kulinda usalama wa Bw. Sharon na maofisa wengine wa serikali.
Rais Katsav alitoa onyo hilo kutokana na maelezo husika ya watu wa kidini. Katika wiki za karibuni, baadhi ya marabi wa dini ya kiyahudi wamezidi kupinga mpango wa upande mmoja, wakidai kuwa kuondoka kutoka eneo la Gaza kumekwenda kinyume cha sheria ya dini ya kiyahudi, na kuwa tishio kwa Israel. Maelezo hayo yanafanana na maelezo ya uchochezi yaliyotolewa na watu wa kidini kabla ya waziri mkuu wa zamani wa Israel Yitzhak Rabin kuuawa. Rais Katsav alikuwa na wasiwasi kuwa, watu wanaopinga mpango huo wanaweza kufikiri kuwa: ili kuepusha Israel iangamizwe, lazima wamuue Bw. Sharon.
Mwaka jana, habari kuhusu watu wenye msimamo wa kulia kutaka kumuua Bw. Sharon ili kuzika mpango wa upande mmoja zilikuwa nyingi. Mwaka huu, maelezo ya nguvu za kulia kumlenga Bw. Sharon yamekuwa mkali zaidi, kama vile zilisema kuwa "Rabin amekufa, pia Sharon lazima afe". Siku kadhaa zilizopita, nguvu za kulia za Israel zilifanya maandamano makubwa, na kuwa na mgogoro mkali na polisi wa Israel. Vitendo hivyo vya nguvu za kulia vimeifanya jamii ya Israel iwe na wasiwasi. Wapelelezi wa idara kuu ya usalama ya Israel tarehe 3 walimtengenezea fulana za kuzuia risasi Bw. Sharon na maofisa wengine wa serikali.
Aidha, kutokana na kuuawa kwa Rabin, inazibidi serikali ya Israel na jamii kuwa macho na jambo hilo. Sio tu idara ya usalama ya Israel kuimarisha ulinzi kwa Bw. Sharon, bali pia rais Katsav alieleza wazi kuwa ana wasiwasi kwa maisha ya Bw. Sharon. Lengo muhimu la kufanya hivyo ni kuionya jamii ya Israel, ili kutoa shinikizo kubwa kwa watu wenye msimamo kali, na kuepusha msiba kutokea tena. Katika hali hiyo, kama watu hao watafanya vitendo, basi uwezekano wa kupata ushindi pia utakuwa mdogo.
Vitendo vya ususiaji wa nguvu za kulia vimepingwa sana nchini Israel, kwa kuwa vitendo hivyo vimetishia usalama wa watu wasio na hatia. Uchunguzi wa maoni ya raia umeonesha kuwa, siku hizi kiasi cha uungaji mkono kwa mpango wa upande mmoja kimeongezeka na kufikia asilimia 63 kutoka asilimia 50 ya wiki zilizopita. Sababu muhimu ni kwamba vitendo vya watu hao vimewakasirisha watu wote. Baadhi ya viongozi wa nguvu za kulia hivi sasa wametambua hatari ya vitendo hivyo kwa wao wenyewe. Mbunge wa nguvu za kulia Bw. Effi Eitam hivi karibuni alisema kuwa, atafanya mazungumzo na wajumbe wa dini, na kutunga mpango wa ususiaji bila ya mabavu, ili kuepusha "msiba" kutokea wakati wa kuondoka kutoka eneo la Gaza.
Hivyo si rahisi kwa watu wenye msimamo mkali kuzusha msiba, lakini bado inahitaji kuwa macho.
Idhaa ya Kiswahili 2005-07-05
|