Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-05 15:49:28    
Mtu anayeendeleza shughuli zake katika dunia nzima

cri

Bw. Hou Weigui ni mkurugenzi wa kampuni ya Zhongxing yenye kiwanda kinachozalisha zana za mawasiliano ya habari, ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa nchini China. Chini ya uongozi wake, kampuni ya Zhongxing ilipata mafanikio mara kwa mara katika soko la kimataifa la zana za mawasiliano ya habari. Walikuza mawasiliano ya habari ya mtandao hadi uwanja wa michezo ya Olimpiki wa Athens, kuuza simu za mkononi hadi kwenye makao makuu ya Nokia na kuendeleza masoko hadi katika nchi na sehemu zaidi ya 60 duniani. Pato la kampuni ya Zhongxing kutokana na mauzo katika nchi za nje lilizidi dola za kimarekani bilioni 1.6. Bw. Hou Weigui ni mpole, yeye ni mwembamba mwenye umri wa miaka 63 mwaka huu. Miaka 21 iliyopita, aliishi katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China, alihamia mkoa maalumu wa Shenzhen ulioko katika sehemu ya kusini ya China baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya 40 na kuwa kiongozi wa kiwanda kimoja kidogo. Chini ya uongozi wake, kiwanda hicho, ambacho kilifanya kazi za usindikaji wa vipuri vya elektroniki, sasa kimekuwa kampuni ya mawasiliano ya habari ya Zhongxing ambayo inaongoza katika sekta ya mawasiliano hapa nchini. Hivi sasa bidhaa za kampuni hiyo zinahusu maeneo matatu ya mawasiliano ya habari ya wireless, mtandao wa mawasiliano ya kompyuta na simu za mkononi. Pato la kampuni hiyo katika mwaka uliopita lilizidi Yuan za Renminbi bilioni 30.

Zaidi ya miaka 10 iliyopita wakati makampuni mashuhuri ya kimataifa ya mawasiliano ya habari yalipoingia kwenye soko la China, kampuni ya Zhongxing iliamua kukuza shughuli zake katika nchi za nje. Wakati ule pato la kampuni ya Zhongxing halikufikia dola za kimarekani milioni 100, lakini pato la kampuni ile ndogo kabisa ya sekta hiyo duniani lilizidi dola za kimarekani bilioni 6 kwa mwaka. Ili kujiepusha kushindana uso kwa uso na makampuni makubwa ya kimataifa, kampuni ya Zhongxing ililenga shabaha kwenye nchi zinazoendelea, ambazo kampuni kubwa za kimataifa zilikuwa bado hazijawekeza sana. Kampuni ya Zhongxing ilianzisha shughuli za biashara katika nchi za Asia ya kusini, kisha katika Afrika, Ulaya ya mashariki hadi baadhi ya nchi za Latin Amerika.

Kwa kulinganishwa na washindani wake, hali bora iliyokuwa nayo kampuni ya Zhongxing ni bidhaa bora, teknolojia ya kisasa lakini bei ya bidhaa zake ni ndogo. Bw. Hou Weigui alisema,

"Hivi sasa tuna wataalamu wenye shahada ya pili na ya tatu zaidi ya 6,000, na watafiti zaidi ya elfu 10, ikiwa washindani wetu wa Ulaya na Marekani wangekuwa na kundi kubwa la watafiti kama hili, wangetumia gharama kubwa sana katika utafiti. Nchini China kuna wahandisi wengi, hivyo katika muda mrefu ujao tutaweza kuwa na hali bora ya teknolojia ya kiwango cha juu pamoja na gharama ndogo ya nguvukazi."

Bw. Hou Weigui alisema kuwa hivi sasa kampuni ya Zhongxing ina wafanyakazi zaidi ya elfu 20, ambao zaidi ya 40% kati yake ni watafiti, mishahara yao ni kutoka Yuan laki 1 hadi laki 5 kwa mwaka, kiasi hiki ni kikubwa nchini China, lakini ni kiasi cha theluthi moja kulinganishwa na mishahara ya wahandisi wa makampuni ya kimataifa.

Baada ya kuingia masoko ya kimataifa, changamoto inayokabili kampuni ya Zhongxing ni utoaji huduma baada ya bidhaa zake kuuzwa kwa wateja. Licha ya kupeleka idadi kubwa ya wahandisi katika nchi hizo, kampuni ya Zhongxing imeweka lengo la kutumia wahandisi wa nchi hizo. Hivi sasa, kampuni hiyo imeajiri wahandisi zaidi ya 1,000, mfumo wa utoaji huduma umeenea kote duniani. Bw. Hou Weigui alisema,

"Kujenga mfumo huo wa huduma ni kweli kutatumia fedha nyingi, lakini tunapaswa kutatua tatizo la utoaji huduma katika nchi hizo ili kuondoa wasiwasi wa wateja. Tumekuwa na mafundi zaidi ya 300 nchini India, na zaidi ya 60% kati yao ni wa huko huko, nchini Pakistan kuna mafundi zaidi ya 400, ambao zaidi ya 70% ni wa nchi hiyo."

Habari zinasema kuwa ili kuinua kiwango cha teknolojia cha mafundi wa nchi za nje, kampuni ya Zhongxing inawapelaka mafundi hao kwenye makao makuu yaliyoko Shenzhen, China kupata mafunzo kila baada ya muda maalumu .

Chini ya uongozi wa Bw. Hou Weigui, masoko ya kampuni ya Zhongxing katika nchi za nje yanapanuka mwaka hadi mwaka na kuingia masoko ya nchi zilizoendelea ambayo yalishikwa na makampuni mashuhuri ya kimataifa ya mawasiliano ya habari.

Meneja mkuu wa masoko ya Ulaya wa kampuni ya Zhongxing Bw. Chen Jiang alisema,

"Zana zetu haziruhusiwi kuingia nchini Ugiriki bila kupitia shirika la mawasiliano ya habari ya Ugiriki(OTE). Mwezi Oktoba mwaka 2002 tulishiriki kwenye maonesho nchini Ugiriki. Kwa bahati nzuri, sehemu yetu ya maonesho ilitazamana na sehemu ya maonesho ya OTE, tulitumia nafasi hiyo na kuwasiliana nao na kuomba wapime zana zetu, matokeo yaliwashangaza sana, kwani zana zetu ni bora zaidi kuliko zao."

Ubora wa bidhaa za China unalingana na bidhaa za Ugiriki, lakini bei za bidhaa za China ni rahisi sana kuliko zao.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-05