Mazungumzo ya viongozi na wafanyabiashara wa nchi za kanda ndogo ya Mto mkubwa wa Mekong tarehe 4 yalifanyika mjini Kunming. Viongozi wa nchi sita kwenye kanda ndogo ya Mto Mekong (Greater Mekong Subregion), China, Kambodia, Laos, Myanmar, Thailand na Vietnam pamoja na mkuu wa benki ya maendeleo ya Asia na wajumbe wa wafanyabiashara jumla ya zaidi ya 300 walihudhuria mazungumzo hayo. Viongozi wa nchi hizo wamesema kuwa watafanya jitihada nyingi zaidi kuimarisha ushirikiano na kuletea mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwenye mazungumzo, mawaziri wakuu wa nchi sita na mkuu wa benki ya maendeleo ya Asia Bw. Kuroda Haruhiko pamoja na wajumbe walijadiliana kwa kina kuhusu kurahisisha uwekezaji, kuboresha miundo mbinu na kuanzisha mtandao wa habari. Kwenye mazungumzo waziri mkuu wa China Wen Jiabao alisifu sana kazi zilizofanywa na wafanyabiashara, akitumai kuwa watashiriki kwa juhudi kubwa zaidi katika maendeleo ya kanda ndogo ya Mto Mekong na kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya uchumi kwa pamoja. Alisema,
"Maingiliano kati ya serikali na wafanyabiashara ni muhimu sana kwa ustawi wa pamoja. Ukweli wa mambo umethibitisha kuwa jambo muhimu la kuongeza nguvu za ushindani za kikanda ni maingiliano kati ya serikali na wafanyabiashara na kusukuma wafanyabiashara washiriki kwenye ushirikiano wa kiuchumi. Mazungumzo hayo yanayofanyika sasa kabla ya mkutano wa pili wa viongozi wa nchi za kanda ndogo, yameonesha nia thabiti ya ushirikiano wa kuendeleza uchumi wa kikanda."
Kuanzisha mtandano wa habari ni mada nyingine muhimu katika mazungumzo hayo. Naibu meneja mkuu wa Shirika la Habari za Mtandao alipohojiwa na waandishi wa habari alisema,
"Kuanzisha mtandao wa habari kutawaletea watu wa nchi sita manufaa makubwa, na pia kutasaidia sana maendeleo ya pamoja ya uchumi, maingiliano ya utamaduni. Kuhusu upashanaji habari wa mtandao China, inaisaidia sana Vietnam, mashirika ya China yamehakikisha teknolojia ya mtandao huo. Katika maendeleo ya upashanaji habari, nchi mbili zinashirikiana katika miradi mingi, na ushirikiano kati ya nchi mbili una nafasi kubwa ya kuendelea."
Ushirikiano wa kilimo ni mada nyingine katika mazungumzo hayo. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara Bw. Kissana Vongsay akiwa mjumbe wa wafanyabishara waliohudhuria mazungumzo alipohojiwa na waandishi wa habari alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huo kwa nchi ya Laos. Alisema,
"Mazao aina 208 ya Laos yamesamehewa au kuondolewa kabisa ushuru. Hivi sasa serikali ya Laos inajitahidi kuwapokea wanamashirika wa China kuwekeza nchini Laos, ninaamini kuwa muda si mrefu baadaye mazao mengi ya Laos yataingia kwenye soko la China."
Wajumbe wa wafanyabiashara wa nchi sita walitoa maoni na mapendekezo yao kuhusu kurahisisha urasimu wa uwekezaji, na kuinua tija ya kazi za serikali. Viongozi wa nchi sita walisema kwamba watazingatia kwa makini maoni na mapendekezo yao na kuyafanya yawe hatua halisi.
Picha husika >>
1 2
|