Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-05 20:36:27    
Kobe-China yahimiza kazi ya kuwafuatilia watu wenye hatari ya kuambukizwa Ukimwi

cri

Mkutano wa 7 wa kimataifa wa Ukimwi wa sehemu ya Asia na Pasifiki umefungwa leo (tarehe 5) huko Kobe, Japan. Naibu waziri wa afya wa China Bwana Wang Longde alihutubia mkutano huo akijulisha hatua zilizochukuliwa na China katika kudhibiti na kutibu ugonjwa wa Ukimwi.

Bw. Wang Longde kwanza alifahamisha hali mbaya inayoikabili serikali ya China katika kukinga na kutibu Ukimwi. Alisema kuwa, serikali ya China inashikilia kanuni ya kufuatilia maisha ya binadamu, inatilia mkazo kazi ya kuwafuatilia watu wenye hatari ya kuambukizwa Ukimwi.

Bw. Wang Longde aliongeza kuwa, baada ya kazi ya kuwafuatilia watu wenye hatari ya kuambukizwa Ukimwi kupata mafanikio kwenye sehemu za majaribio, maarifa mazuri yataenezwa haraka nchini. Serikali ya China pia imeunda vikundi vya watu wanaoingilia kati watu wenye hatari ya kuambukizwa Ukimwi katika mashirika mbalimbali ya udhibiti wa magonjwa, na kuyahimiza mashirika ya kienyeji kushughulikia kazi hiyo.