Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-06 15:55:45    
Kazi maalum ya tiba ya ya kichina na mitishamba ya kichina katika kutibu ugonjwa wa ukimwi

cri

Hivi sasa, ugonjwa wa ukimwi ni tatizo kubwa linalolikabili suala la afya ya umma duniani. Kutokana na jududi zilizofanywa katika zaidi ya miaka 20, binadamu wamepata uzoefu mkubwa katika kutibu ugonjwa huo, lakini mpaka sasa, ugonjwa huo bado hautibiki. Mpaka sasa, kwa ujumla, watu milioni 23 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Hivi sasa, wanasayansi wa udaktari wa nchi mbalimbali duniani wanafanya juhudi katika kutafuta tiba ya ugonjwa wa ukimwi, wamegundua kuwa tiba ya kichina na mitishamba ya kichina ikiwa ni tiba ya jadi, inaweza kufanya kazi kubwa katika kutibu ugonjwa wa ukimwi, ikilinganishwa na dawa za kimagharibi mitishamba ina kazi yake maalum katika kutibu ugonjwa huo.

Tangu miaka ya 80 ya karne iliyopita, ugonjwa wa ukimwi ulikuwa umeanza kuenea barani Afrika, ambapo tiba ya kichina na mitishamba ya kichina ilikuwa imeanza kutumika.

Mwaka 1987, aliyekuwa rais wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi alifanya ziara nchini China, ambapo alitumai kuwa China itawapeleka wataalamu wa tiba ya kichina nchini Tanzania kuisaidia kutibu ugonjwa wa ukimwi. Serikali ya China ilikubali ombi lake. Muda mfupi baada ya hapo, China na Tanzania zilianzisha mradi wa ushirikiano wa kutibu ugonjwa wa ukimwi kwa tiba ya kichina na mitishamba ya kichina. Ofisa wa idara ya usimamizi wa tiba ya kichina na mitishamba ya kichina Bw. Yang Longhui alifahamisha mradi huo akisema:

"Mradi huo uliosainiwa na serikali za China na Tanzania umesifiwa na watu wengi. Hivi ssasa mradi huo bado unaendelea? na serikali ya Tanzania inaitaka China iongeze muda wa utekelezaji wa mradi huo mara kwa mara."

Imefahamika kuwa katika miaka 18 iliyopita, wataalamu wa China wamewatibu wagonjwa karibu elfu 10 wa ukimwi, kati ya asilimia 40 hadi asilimia 52 ya wagonjwa hao wamepata nafuu kwa viwango tofauti, miongoni mwa wagonjwa waliotibiwa kabla ya mwaka 1990, asilimia 10 kati yao bado wako hai.

Katika miaka ya karibuni, ugonjwa wa ukimwi umeanza kuenea hapa China, hivi sasa wagonjwa wengi wa ukimwi wanatibiwa kwa njia ya tiba ya kimagharibi, ambayo ni njia iliyopevuka na inayotumika sana duniani. Mpaka mwaka 2004, China ilichagua mikoa na miji 11 kama vituo vya majaribio vya kuwatibu wagonjwa wa ukimwi kwa kutumia tiba ya kichina, na wagonjwa wa ukimwi na watu walioambukizwa virusi vya ukimwi elfu 7 wametibiwa.

Mkoa wa Henan, katikati ya China, ni moja ya mikoa iliyoanzisha vituo vya majaribio ya kuwatibu wagonjwa wa ukimwi kwa tiba ya kichina na mitishamba ya kichina. Anayeshughulika na kazi hiyo Bw. Xu Liran, alisema:

"Hivi sasa wagonjwa 1792 wa ukimwi mkoani Henan wanatibiwa kwa tiba ya kichina na mitishamba ya kichina, wakiwemo wagonjwa wa ukimwi na watu walioambukizwa virusi vya ukimwi ambao hawafai kutibiwa kwa njia ya tiba ya kimagharibi, kutokana na hali yao isiyo mbaya ya maradhi mengine yaliyowapata, na wagonjwa wa ukimwi ambao njia ya tiba ya kimagharibi itawaletea madhara.

Kuna tofauti kubwa kati ya tiba ya kichina na tiba ya kimagharibi katika kutibu ugonjwa wa ukimwi. Lengo la tiba ya kimagharibi ni kupunguza virusi mwilini kwa kuviua, lakini lengo la tiba ya kichina ni kuongeza uwezo wa mwili wenyewe wa kujikinga na virusi vya ukimwi, kwa msingi huo, njia mbalimbali zinatumika kupunguza dalili za ugonjwa huo.

Baada ya kuambukizwa virusi vya ukimwi, dalili mbalimbali zinatokea siku hadi siku kwenye mwili wa binadamu, kama vile, kupungua uzito, kuharisha, homa, maumivu ya kichwa, kutokuwa na hamu ya kula, hata kuvimba kwa mafindofindo au kuwa na kifua kikuu. Sababu za kutokea kwa dalili hizo ni za kutatanisha, tiba ya kimagharibi haiwezi kuzitibu, lakini tiba ya kichina inaweza kupunguza dalili hizo kwa kiasi kikubwa, na kupunguza maumivu ya wagonjwa. Daktari mmoja mzee wa tiba ya kichina wa mkoa wa Henan Bw. Li Fazhi alifahamisha akisema:

"Kabla sijaja kwenye kijiji hicho, wagonjwa wa ukimwi wa huko walikuwa wana dalili nyingi za ugonjwa, kama homa na kifua kikuu, baada ya kutibiwa, dalili hizo hizo zimepunguzwa, hali ambayo imewaridhisha."

Ingawa tiba ya kichina na mitishamba ya kichina ina kazi maalum katika kutibu ugonjwa wa ukimwi, lakini ina matatizo fulani, kwa mfano, kutokana na kutokuwa na vigezo vya pamoja kwenye majaribio ya tiba ya kichina, ni vigumu kutambulika kwa takwimu zinazotoka majaribio hayo; na hakuna mfumo wa pamoja wa kuthibitisha kazi ya tiba ya kichina. Hali hizo ni vikwazo kwa maendeleo ya kazi ya kutibu ugonjwa wa ukimwi kwa tiba ya kichina na mitishamba ya kichina.

Ili matibabu ya kichina na mitishamba ya kichina iweze kufanya kazi yake vizuri katika kutibu ugonjwa wa ukimwi, hivi sasa China inafanya juhudi katika kutafiti na kuweka vigezo vya majaribio ya tiba ya kichina na mfumo wa kuthibitisha kazi ya tiba hiyo, ili kuweka msingi kwa kueneza kazi ya kutibu ugonjwa wa ukimwi kwa tiba ya kichina.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-06