Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-06 18:57:06    
Mapishi ya kukoroga bilinganya kwa mchuzi

cri

Mahitaji

mabilinganya gramu 500, nyama ya kusagwa gramu 100, chumvi gramu 5, siki gramu 10, M.S.G gramu 5, sukari gramu 5, mchuzi wa soya gramu 10, vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi kila kimoja gramu 5.

Njia

1. Osha mabilinganya halafu ondoa gamba lake. yapasue mabilinganya yawe vipande vipande, vipakue ndani ya sahani. Pasha moto, mimina maji kwenye sufuria, weka sahani hiyo kwenye sufuria, chemsha kwa dakika 8 mpaka yawe laini. yakaushe, tia chumvi, sukari, siki korogakoroga. Kisha ondoa na kuyawekea kwenye friji.

2. pasha moto tena tia mafuta kidogo kwenye sufuria mpaka nyuzi 60, tia nyama ya kusagwa, korogakoroga , mimina mchuzi wa soya na maji kidogo, na tia chumvi na M.S.G, ipakue na uiwekee kwenye vipande vya bilinganya. Tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi. Korogakoroga, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari. Na kinafaa zaidi kuliwa wakati wa majira ya joto.