Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-07 16:26:23    
Mji wa London umeshinda na kuwa mwenyeji wa kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka 2012

cri

Tarehe 19 Juni, saa moja na dakika 45 jioni kwa saa za Singapore, mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki Bw. Jacques Rogge alitangaza: "Mwenyeji wa kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka 2012 ni London". Hadi hapo shughuli mfululizo za kuwania nafasi ya kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki mwaka 2012 kwa kueleza, kupima na kupiga kura zilikuwa zimekamilika.

Miji iliyowania nafasi ya kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka 2012 ni London, Paris, New York, Madrid na Moscow. Mwishowe Londo imewashinda wapinzani wake na kupata nafasi ya kuandaa michezo hiyo. Hii ni mara ya tatu kwa mji wa London kuandaa michezo hiyo baada ya mwaka 1908 na 1948.

Kutokana na katiba ya Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki, mji uliopata zaidi ya nusu ya idadi ya kura ndio unaopata haki ya kuandaa michezo hiyo, ikiwa miji yote haikupata zaidi ya nusu ya idadi ya kura, mji uliopata kura chache unatolewa, na miji iliyobaki itapigiwa kura kwa duru nyingine mpaka kupata mji uliopata zaidi ya nusu ya idadi ya kura.

Lakini katika maduru matatu ya mwanzo, miji yote mitano ilikaribiana sana katika idadi ya kura, na hakuna mji hata mmoja uliozidi nusu ya idadi ya kura. Mji wa Moscow ulitolewa katika duru la kwanza, na mji wa New York ulitolewa katika duru la pili. Katika duru la tatu mji wa Madrid uliokuwa unategemea sana kupata ushindi pia ulitolewa kwa kukosa kura mbili tu. Katika duru la mwisho mji wa London uliushinda mji wa Paris kwa kura za 54 kwa 50.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki Bw. Jacques Rogge alitoa pongezi kwa London na kutoa heshima kwa Paris, New York, Madrid na Moscow, akitumai kuwa miji hiyo haitaacha juhudi za kugombea nafasi hiyo katika safari ijayo.

Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya London ilieleza kuwa itawasilisha katiba husika kwenye bunge la Uingereza, na idara husika zitaanza kufanya zabuni kwa ajili ya miundo mbinu ya michezo ya Olimpiki. Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya London ambaye pia alikuwa bingwa katika mashindano ya mbio za mita 1500 katika mwaka 1980 na 1984 Bw. Sebastian Coe alisema, kwa ufahari London imepata nafasi ya kuwa mwenyeji wa kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka 2012, London haitaisikitisha familia ya Olimpiki na haitasahau jukumu lake la kimataifa na inatumai vijana wote duniani watashiriki kwenye michezo ya riadha.

Katika uchaguzi huo, Paris ilikuwa ikitazamiwa sana kuwa mshindi, na hata baadhi ya vyombo vya habari vilibashiri kuwa Paris hakika itashinda. Kushindwa kwa Paris kuliwashitusha sana wanakamati wengi wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki. Mwanakamati wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki, ambaye pia ni mwenyekiti wa idara ya kupinga matumizi ya dawa za kuongeza nguvu duniani Bw. Dick Pound alisema, kuna sababu nyingi zilizosababisha London ishinde na Paris ishindwe.

Bw. Pound alisema, sababu ya Londo kushinda katika uchaguzi ni kuwa London inashikilia kueneza moyo wa michezo ya Olimpiki kwa kila kijana duniani katika mchakato mzima wa kuwania nafasi ya kuandaa michezo ya Olimpiki. Aliongeza kuwa, licha ya London kushikilia kuenzi moyo wa michezo ya Olimpiki, na Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya London chini ya uongozi wa Sebastian Coe kuandaa mpango wa kila kitu, serikali ya London pia ilifanya juhudi kubwa kwa ajili ya ushindi huo.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-07