Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-07 16:45:47    
Maelezo mafupi kuhusu Tibet

cri

Mkoa unaojiendesha wa Tibet ni sehemu ambayo wako watu wa kabila la Tibet. Mkoa huo uko sehemu ya kusini magharibi mwa uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet. Kaskazini unapakana na mkoa wa Qinghai na Xinjiang, kusini mashariki unapakana na mkoa wa Yunnan, kusini na magharibi unapakana na nchi na sehemu kadhaa zikiwemo India, Nepal, Bhutan, Myanmar, mashariki unapakana na mkoa wa Sichuan. Uko kati ya latitudo ya kaskazini 26'52" hadi 36'32" na longitudo ya mashariki 78'24" hadi 99'06". Eneo lake ni kilomita za mraba milioni 1.22, ambalo linachukua moja ya nane la eneo lote la ardhi ya China. Idadi ya watu mkoani humo ni milioni 2.36, miongoni mwao asilimai 95.5 ni Watibet. Pia kuna watu wa makabila mengine, wakiwemo Wamenba, Waluoba, Wahan, na Wahui. Mji mkuu wa mkoa wa Tibet ni mji wa Lhasa.

Mkoa wa Tibet uko katika uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet wenye mita 4000 juu ya usawa wa bahari, na unasifiwa kuwa paa la dunia. Wastani wa urefu kutoka usawa wa bahari wa Mlima Himalaya ni zaidi ya mita elfu 6, na kilele chake cha Mlima Qomolangma kina urefu wa mita 8848.13, ambacho ni kilele kirefu zaidi duniani. Mlima Gangdisi una urefu wa mita 5500 hadi mita 6000 kutoka usawa wa bahari, urefu wa kilele chake Gangrenboqi ni mita 6656, ambacho kinasifiwa kuwa mlima mtakatifu. Kusini ya Mlima Gangdisi kuna Mlima Nianqing Tangla ambao una urefu kati ya mita 4500 hadi 5000 kutoka usawa wa bahari, kilele chake ni chenye urefu wa mita 7111. Wastani wa urefu kutoka usawa wa bahari wa Mlima Tangla ni mita 5500 hadi mita 6000, na kilele chake Geladadong ni chenye urefu wa mita 6621.

Kutokana na sababu za kijiografia, kihistoria na mawasiliano, katika muda mrefu uliopita, ufugaji ulikuwa sekta muhimu ya kiuchumi mkoani humo. Msingi wa uchumi na uwezo wa uzalishaji uko nyuma. Kutokana na maendeleo yaliyopatikana miaka ya karibuni katika mageuzi na ufunguaji mlango, biashara na nchi za nje na utalii ulivyoendelea, uchumi na ujenzi wa miji na vijiji mkoani Tibet umekua kwa kiasi kikubwa.

Sehemu ya Linzhi iko sehemu ya chini ya Mto Yaluzangbu, wastani wa urefu kutoka usawa wa bahari ni mita 3000 hivi. Mvua ni yakutosha na mandhari ya kupendeza. Miji na vivutio muhimu vya kitalii ni pamoja na eneo la kiuchumi la bonde la Mto Niyang, mji wa Bayi, kivutio cha kitalii cha mto Palongzangbu. Mji wa Bayi ulioko kando ya Mto Niyang ni kituo cha kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wa sehemu hiyo.

Sehemu ya Linzhi inajulikana kwa kuwa na bonde kubwa lenye kina kirefu zaidi duniani. Huko kuna mimea na wanyama adimu, na kutokana na sehemu hiyo kuwa mbali na makazi ya watu, hali ya kimaubile inahifadhiwa vizuri.

   

picha husika>>

1  2  3