Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-08 14:21:05    
Kampuni ya Betri ya Anyang mkoani Henan yaendeleza shughuli zake barani Afrika

cri

Betri ndogo ziliposaidia mashirika ya China kuingia kwenye soko la Afrika, pia zimeleta nafasi za ajira na ongezeko jipya la uchumi. Ushirikiano huo wa kunufaishana umesifiwa na serikali na viongozi wa nchi hizo mbili.

Naibu mkuu wa Kiwanda cha betri cha Anyang Bwana Wang Tiancheng alimwambia mwandishi wa habari wa Shirika la habari la Xinhua kuwa, tokea mwaka 1993, wamefanya juhudi za kuanzisha shughuli zao barani Afrika, ambapo wameanzisha "Kampuni ya kimataifa ya Jinzhong" na "Kiwanda cha Betri cha Jinzhong" nchini Kenya, kwa ujumla kiwanda cha betri cha Anyang kimepata mapato ya fedha za kigeni za dola za kimarekani karibu milioni 20. Hasa katika miaka kadhaa ya hivi karibuni, mapato ya fedha za kigeni ya kiwanda hicho yanafikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 6 kwa mwaka.

Bwana Wang Tiancheng alisema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, mahitaji ya betri kwenye soko la Afrika yamekuwa makubwa siku hadi siku, mauzo ya betri za saizi A na saizi AA za China kwenye soko la Afrika yamechukua asilimia 80 ya mauzo ya jumla ya kiwanda hicho. Mauzo ya betri za chapa ya Kifaru za Anyang, China si kama tu yamechukua zaidi ya asilimia 40 kwenye soko la Kenya, bali pia yameingia kwenye masoko ya Uganda, Tanzania, Somalia na Ethiopia.

Bwana Wang Tiancheng alisema, hivi sasa wanafanya mpango wa kukusanya fedha ili kupanua jengo la kiwanda chao nchini Kenya na kuongeza mistari mitano ya uzalishaji bidhaa, wakati huo huo wataanzisha ofisi yao nchini Gambia ili kuanzisha shughuli zao kwenye soko la Afrika ya magharibi.

Mwaka 1993, wakati bidhaa za betri zilipokuwa nyingi kupita kiasi cha mahitaji kwenye soko la nchini China, ambapo kiwanda cha betri cha Anyang kilipokabiliwa na hali hatari ya kuwepo kwake, baada ya kufanya ukaguzi na kuthibitisha kwa makini, kiwanda cha betri cha Anyang kiliamua kuanzisha shughuli zake barani Afrika. Kwa upande mmoja, walifahamishwa kuwa idadi ya watu wa Afrika ni kubwa, lakini uchumi wa nchi za Afrika bado uko nyuma, ambapo kuna ukosefu mkubwa wa umeme na nishati ya moto, hivyo betri zinakaribishwa sana kwenye soko la Afrika, lakini viwanda vya betri vilikuwa vichache barani Afrika, nchi nyingi zilitegemea kuagiza bidhaa za betri kutoka nje. Na kiwanda cha betri cha Anyan kilisifiwa kwa bidhaa zake za betri zilizouzwa barani Afrika kwa miaka mingi.

Kwa kutegemea bidhaa zenye sifa nzuri, Kampuni iliyoanzishwa na Kiwanda cha Betri cha Anyang nchini Kenya imeendeleza shughuli zake za kuuza bidhaa za aina nyingi badala ya bidhaa za betri tu kwenye soko.

Mwaka 1997, serikali ya Kenya ilitoa sera ya kuhamasisha mashirika ya nchi za nje yaanzishe viwanda nchini humo. Kiwanda cha betri cha Anyang kilijipatia mitaji ya ushirikiano wa ubia kutoka kwa serikali ya China, kikaanzisha kiwanda cha kuunda globu huko Nairobi, Kenya, ambacho kwa siku kinatengeneza globu elfu 50, baadaye kilianzisha kiwanda cha betri na kiwanda cha kutengeneza tochi.

Mwaka 2002, chini ya msaada wa wizara ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nje ya China, kiwanda hicho kilijenga kiwanda kipya chenye mistari 6 ya uzalishaji bidhaa kwenye sehemu ya uuzaji bidhaa nje na utengenezaji bidhaa ya Mto Athi nchini Kenya, ambapo kinatengeneza betri za saizi A, saizi AA, tochi na bidhaa nyingine.

Bwana Wang Dacheng alisema, upande wa Kenya unakaribisha sana uwekezaji wa kampuni za China na ushirikiano wao, imezitolea sera nafuu, wafanyakazi wenyeji zaidi ya 150 walioajiriwa na kiwanda hicho wanathamini sana nafasi zao za ajira, wanachapa kazi sana, tena kiwanda hicho kina utaratibu kamili wa uendeshaji, hivyo ufanisi wake ni mzuri ambao unachangia ongezeko la uchumi wa Kenya.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-08