Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-08 16:27:08    
Milipuko kadhaa ilitokea mjini London na kusababisha vifo vya watu wengi na wengine kujeruhiwa

cri

Tarehe 7 asubuhi saa za kwenda kazini milipuko kadhaa ilitokea mjini London kwenye subway na mabas. Polisi ya Uingereza imethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa katika milipuko hiyo imeongezeka na kufikia 38 na majeruhi wamezidi mia 7, kati yao watu miongo kadhaa wako katika hospitali na hali zao ni mahututi.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika kituo cha subway Aldgate East mjini London. Msafiri mmoja alisema, mlipuko ulitokea katika behewa lililokuwa jirani na behewa lake, wakati huo subway ilikuwa ikienda, taa zote zilizimika, na subway lilisimama ghafla na moshi mnene ulienea ndani ya njia ya subway, watu walikohoa kwa nguvu wakisubiri misaada kutoka nje.

Kisha, mara mlipuko mwingine ulitokea kwenye mabasi. Mmoja aliyesalimika katika mlipuko huo alisema, wakati huo alikuwa ndani ya ghorofa ya basi, ghafla mngurumo mkali wa kutia kiziwi ulisikika na alipoangalia juu akiona mbingu buluu, paa la basi lilifumuliwa kabisa.

Kwenye sehemu ya matukio, watu wote hawaruhusiwi kuondoka kabla ya kusachiwa na polisi, inspekta mmoja alisema, serikali imeanzisha mpango wa kupambana na dharura, na hali imedhibitiwa.

Kutokana na tukio hilo la ghafla mawasiliano ya simu za mkononi yaliongezeka kasi na simu nyingi zilikuwa na tatizo. Msemaji wa Shirika la Simu za Mikononi Vodafone alisema, shirika lake limefungua huduma maalumu wakati wa dharura, na alitaka watu wasiokuwa na shida ya haraka wasitumie simu za mkononi ili kuwaachia wenye shida za dharura.

Hapo mapema baada ya milipuko kutokea, polisi ilisema milipuko ilisababishwa na tatizo la umeme, lakini tovuti moja ya mtandao wa internet ya Kiislamu ilitangaza kuwa milipuko ilifanywa na "Jumuyia ya Siri ya al-Qaeda Barani Ulaya".

Wakati milipuko ilipotokea, viongozi wa kundi la nchi nane tajiri, G 8, pamoja na nchi nyingine tano zinazoendelea walikuwa wakifanya mkutano huko Scotland, kaskazini mwa Uingereza. Dakika chache baada ya kutokea kwa milipuko, waziri mkuu wa Uingereza Bw. Blair alitoa taarifa ya kulaani akisema, tukio hilo ni la "kishenzi" na kusema hayo ni "mashambulizi ya kigaidi". Baada ya mkutano wa dharura mjni London Bw. Blair alisema kuwa Waingereza hawatatishiwa na magaidi. Hivi sasa polisi ya Uingereza imefanya uchunguzi mkali na kujitahidi kuwagundua kwa haraka na kuwaadhibu kisheria magaidi hao.

Baada ya milipuko kutokea mjini London, jumuyia ya kimataifa ililaani vikali tukio hilo na kuonesha kuwa itaungana pamoja katika mapambano dhidi ya ugaidi. Baada ya kujadiliana, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kulaani laana kwa tukio hilo la milipuko mjini London, na kusema kuwa kitendo chochote cha ugaidi ni tishio kwa amani na usalama.

Msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China alisema kuwa China inalaani tukio hilo la milipuko, na kusema kuwa China inapinga kithabiti ugaidi, na inapenda kushirikiana na jumuyia ya kimataifa katika ushirkiano dhidi ya ugaidi.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, nchi nane tajiri na nchi tano zinazoendelea mara zilitoa taarifa ya pamoja kulaani tukio hilo na kusema kuwa mashambulizi hayo ya kigaidi hayakulenga nchi moja tu bali nchi zote na jamii ya ustaarabu. Rais wa Ufaransa Chiraq kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, tukio la milipuko mjini London sio tu limeimarisha umoja wa kundi la nchi nane na pia limeimarisha umoja kati ya kundi la nchi nane na nchi tano zinazoendelea kwenye mkutano huo.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-08