Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-08 17:55:26    
Mashambulio makubwa ya kigaidi yaliyotokea duniani katika miaka ya karibuni

cri

Tarehe 7 mwezi Julai asubuhi, milipuko kadhaa ilitokea katika vituo vya sabwe na mabasi mjini London, na kusababisha vifo vya watu wengi. Yafuatayo ni mashambulio makubwa yaliyotokea duniani baada ya tukio la tarehe 11 mwezi Machi mwaka 2004 nchini Hispania.

Tarehe 12 mwezi Juni mwaka 2005, milipuko kadhaa ilitokea huko Tehran, mji mkuu wa Iran na Ahvaz, mji mkuu wa mkoa wa Kuzestan, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 10, na wengine 80 kujeruhiwa.

Tarehe 28 mwezi Mei mwaka 2005, watu kadhaa wenye silaha walitupa mabomu ya mkono katika soko moja mjini Srinagar, Kashmir, na kuwajeruhi watu wasiopungua 14. Na siku hiyo mlipuko wa mabomu yaliyowekwa ndani ya gari uliotokea mbele posta moja mjini Anantnag kusini ya Srinagar, na kuwajeruhi watu wasiopungua 16.

Tarehe 27 mwezi Mei mwaka 2005, mjini Islamabad nchini Pakistan mlipuko uliotokea katika kaburi moja la watakatifu wakati sherehe ya kidini ilipofanyika, na kusababisha vifo vya watu 20 na watu karibu mia moja kujeruhiwa.

Tarehe 28 mwezi Februari mwaka 2005 asubuhi, shambulio la kujiua lilitokea mjini Hillah kusini ya Baghdad. Mtu aliyeanzisha shambulio hilo aliendesha gari lenye mabomu na kuingia msururu wa watu waliokuwa wanaomba kupata ajira katika idara za serikali na kuzusha mlipuko, ambao ulisababisha vifo vya watu wasiopungua 110 na watu 200 kujeruhiwa.

Tarehe 25 mwezi Februari mwaka 2005 usiku, mlipuko wa kujiua ulitokea mjini Tel-aviv, Israel, na kusababisha vifo vya watu wanne na 28 kujeruhiwa.

Tarehe 30 mwezi Januari mwaka 2005, wakati upigaji kura wa uchaguzi mkuu wa Iraq unapofanyika, mashambulio kadhaa dhidi ya upigaji kura yalitokea nchini humo. Mjini Baghdad tu yalitokea mashambulzi 9, na kusababisha vifo vya watu 29 na wengine 49 kujeruhiwa. Nyumba ya waziri wa sheria pia ilishambuliwa, mlinzi mmoja aliuawa na watu wanne kujeruhiwa.

Tarehe 7 mwezi Oktoba mwaka 2004 usiku, mashambulio matatu dhidi ya Waisrael yalitokea huko Sinai, Misri, na kusababisha vifo vya watalii wasiopungua 35 kutoka Israel kuuawa na watu zaidi ya 160 kujeruhiwa.

Tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 2004, katika siku ya kuadhimisha mwaka wa 135 tangu baba wa taifa wa India Mahatma Gandhi kuzaliwa, milipuko ilitokea mikoani Nagaland na Assam kasikazini mashariki mwa India, na kusababisha vifo vya watu 44 na watu zaidi ya mia moja kujeruhiwa.

Tarehe 1 mwezi Septemba mwaka 2004, watu wenye silaha zaidi ya 30 walikalia shule ya sekondari ya No. 1 katika mji wa Beslan nchini Jamhuri ya Ossetia ya Kaskazini, na kuwateka nyara wanafunzi, wazazi wao na walimu wapatao 1200 waliohudhuria sherehe ya kufungua shule. Katika tukio hilo watu 334 waliuawa, na watu zaidi ya 700 kujeruhiwa.

Tarhe 24 mwezi Agosti mwaka 2004 usiku, ndege mbili za abiria zilizoruka kutoka uwanja wa ndege wa Domodedovu zilianguka mkoani Tula na Rostov, na kusababisha vifo vya watu 89.

Tarehe 21 mwezi Juni mwaka 2004 usiku hadi tarehe 22 alfajiri, watu wenye silaha wa Chechenya wapatao 200 walishambulia majengo 15 ya serikali, jeshi na wananchi nchini Jamhuri ya Ingushetia, na kusababisha vifo vya watu 92, na watu zaidi ya 120 kujeruhiwa. Kaimu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Abukar Koshtoyev aliuawa katikamashambulio hayo.

Tarehe 29 mwezi Mei mwaka 2004 asubuhi, watu kadhaa wenye silaha walishambulia kampuni za mafuta za nchi za nje na makazi ya watu huko Khobar, Saudi Arabia. Waliwaua watu 16, na kuwateka nyara watu zaidi ya 40. baada ya siku mbili, kikosi cha usalama cha Saudi Arabia kilifanikiwa kuwaokoa watu waliotekwa nyara.

Tarehe 9 mwezi Mei, wakati Russia iliposherehekea mwaka wa 59 tangu ushindi wa vita vya kulinda taifa, mlipuko ulitokea katika uwanja wa michezo huko Grozny, Chechenya. Rais Akhmad Kodyrov wa Chechenya na mkuu wa kamati ya mambo ya taifa Bw. Khusein Isayev waliuawa.

Tarehe 11 mwezi Machi mwaka 2004, kabla ya uchaguzi mkuu wa Hispania, milipuko 13 ilitokea katika vituo vitatu vya garimoshi. Kutokana na takwimu za serikali ya Hispania, watu 192 waliuawa, na watu zaidi ya 1500 kujeruhiwa. Baada ya miezi 9, mhalifu aliyeanzisha milipuko hiyo Hassan El Haski alikamatwa na polisi wa Hispania.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-08