Kutokana na mwaliko, rais Hu Jintao wa China alifanya ziara ya kiserikali nchini Russia na Kazakhstan, kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Astana, na mazungumzo ya kundi la nchi 8 na viongozi wa nchi tano za China, India Brazil, Afrika ya Kusini na Mexico. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Zhaoxing leo akiwa njiani kurejea nyumbani alipohojiwa na waandishi wa habari waliofuatana na ujumbe alisema kuwa, ziara hiyo ya rais Hu Jintao imeimarisha uaminifu wa kisiasa, ushirikiano wa kunufaishana na kuhifadhi utulivu wa kikanda.
Bw. Li Zhaoxing alisema kuwa ziara ya rais Hu Jintao inahusiana na mambo mengi yakiwa ni pamoja na urafiki na nchi jirani pamoja na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na mataifa makubwa na nchi muhimu zinazoendelea. Kwa jumla mafanikio ya ziara hiyo yanaonekana katika pande tatu.
Kwanza, kuimarisha urafiki na nchi jirani na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati. Katika miaka ya karibuni uhusiano kati ya China pamoja na Russia na Kazakhstan uliendelezwa katika kipindi kipya. Rais Hu Jintao alipotembelea nchi hizo mbili yeye na rais Putin walisaini "taarifa ya pamoja ya China na Russia kuhusu utaratibu wa kimataifa wa karne ya 21". Rais Hu Jintao na rais Nazarbayev wa Kazakhstan walitangaza kujenga uhusiano wa ushirikiano mpya kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili katika maeneo mbalimbali. China na Russia, na China na Kazakhstan zilisaini nyaraka kadha wa kadha kuhusu ushirikiano wa nishati, mambo ya fedha, umeme na mawasiliano, ambazo zinathibitisha kuwa thamani ya biashara kati ya China na Russia itafikia dola za kimarekani bilioni 60 hadi 80 katika mwaka 2010 na uwekezaji wa China nchini Russia utafikia dola za kimarekani bilioni 12 ifikapo mwaka 2020. Zimesema kuwa thamani ya biashara kati ya China na Kazakhstan itafikia dola za kimarekani bilioni 10, lengo ambalo linahimiza ushirikiano halisi wa pande hizo mbili. Nyaraka hizo zinataka kuimarishwa kwa maingiliano ya kiutamaduni, China na Russia zitaanzisha kwa mbalimbali "Mwaka wa Taifa" ili kuimarisha maingiliano ya sehemu za mipakani mwa nchi hizo mbili. China na Kazakhstan zitaimarisha ushirikiano wa utamaduni na elimu. Viongozi wa nchi mbili za Russia na Kazakhstan walisema kuwa mafanikio aliyopata Bw. Hu Jintao katika ziara yake hiyo yataweka msingi imara kwa uhusiano wa kirafiki na wa kunufaishana kati ya China na Russia, na kati ya China na Kazakhstan katika karne ya 21, na kupeleka uhusiano wa pande mbili katika kipindi kipya.
Pili, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuhimiza maendeleo kwa pamoja. Baada ya kuendelezwa kwa miaka minne, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai imefanya kazi muhimu sana kwa ushirikiano wa usalama na uchumi wa kikanda.
Tatu. Kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na kukabiliana na changamoto kwa njia mwafaka. Kutokana na kukabiliwa na migogoro mingi, kupanuka kwa tofauti kati ya nchi tajiri na maskini, ugaidi na kuharibika vibaya kwa mazingira ya asili hivi sasa duniani, Bw. Hu Jintao anasema kuwa tunapaswa kujitahidi kwa pamoja kudumisha ongezeko la uchumi wa dunia na kuanzisha ushirikiano halisi.
Yaliyo muhimu zaidi ni kuwa Bw. Hu Jintao alipendekeza na kushiriki kwenye mkutano na viongozi wa nchi za India, Brazil, Afrika ya kusini na Mexico na kutoa maoni kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kusini na kusini na kuleta maendeleo kwa pamoja, katika mkutano wao alitoa mapendekezo manne, ambayo yanaonesha kuwa China ni moja ya nchi zinazoendelea na kulinda maslahi ya haki ya nchi zinazoendelea.
Idhaa ya Kiswahili
|