Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-08 21:06:04    
Wushu--Gongfu ya China

cri

Wushu ni urithi bora wa utamaduni wa taifa la China, na pia ni moja ya michezo ya ridhaa ya jadi ya taifa. Na inapendwa sana na wananchi wengi. Katika muda mrefu wa ukuaji wake, wushu imeunda njia ya kujizoeza na mitindo ya maonyesho ya kipekee. Thamani yake ya kujenga afya, ustadi waupigana na sifa yake zimetambuliwa na watu wengi mashuhuri duniani. Tangu zama za kale China ilikuwa ikichukua wushu kama njia ya kujenga mwili, kulinda dhidi ya mashambulizi ya adui na kuchagua askari shujaa. Tangu karne ya 7 katika Enzi ya Tang, China ilianzisha mfumo wa kuchagua ofisa kwa mtihani na mashindano ya wushu. Katika Enzi ya Song kulikuwa vipimo vya mashindano ya wushu kwa kupigana kwenye jukwaa maalumu. Hadi Enzi ya Ming, wushu iliendelezwa sana baada ya mashindano, pia maandishi, na vyombo vya wushu vilikusanywa kwa utaratibu, kwa mfano "kitabu cha matayarisho ya wushu" na maandishi ya ofisa maarufu Qi Jiguang katika Enzi ya Ming vimekuwa kama kamusi ya wushu ya China. Katika Enzi ya Qing mashindano ya wushu yaitwayo "kupigana kwenye jukwaa maalumu" yalienezwa sana miongoni mwa wenyeji. Baada ya kuasisiwa kwa China Mpya, wushu iliorodheshwa katika aina ya michezo ya ridhaa ya mashindano. Licha ya kushindana katika michezo ya kitaifa inayofanywa kila muda maalumu, pia mashindano ya kitaifa ya aina 7 ya wushu yanafanyika.

Ili kuifanya wushu kuwa aina mpya ya michezo ya ridhaa ya dunia, tangu mwaka wa 1983 China ilianza kuipeleka duniani kwa hatua na mpango, kupeleka kwa mfululizo timu za mchezo huo na vikundi vya makocha kwenye nchi mbalimbali kufanya maonyesho na kufundisha. Pia kila mwaka hupokea mashabiki wa wushu wengi wa ng'ambo kuja China kujifunza. Sasa mashirika mengi ya wushu yameundwa katika nchi na maeneo mengi ya mabara matano. Asia, Ulaya, Amerika ya Kusini na Oceania zimeunda jumuiya za wushu za mabara na pia kufanya mashindano ya mwaliko ya wushu ya kimataifa mara tatu. Tangu mwaka 1990 michezo ya XI ya Asia iliorodhesha rasmi wushu kuwa mchezo wa kushindana, na kuanzisha shirikiano la wushu la kimataifa lenye nchi wanachama 38.

Wushu ya China imegawanyika katika makundi mengi na aina nyingi za uchezaji, kwa hivyo jinsi ya kupata vipimo sawa vya mashindano ya wushu ni jambo muhimu la kutanzuliwa. Kutokana na agizo la shirikisho la wushu la Asia, jumuiya ya wushu ya China na chuo cha utafiti wa wushu viliwataka wataalamu wafanye utafiti mwingi, hatimaye walichagua njia 7 za kuwakilishwa katika mashindano, nazo ni ngumi ndefu, ngumi za kusini, ngumi za taiji, ustadi wa utumiaji wa mapanga, mkuki, sime na fimbo. Kila njia inachukua ubora wake, kuondoa vitendo vigumu, na kubakiza staili na tabia maalumu na pia kuzingatia kiwango cha sasa cha wanamichezo wa nchi mbalimbali. Njia hizo zimekubaliwa na makocha na wanamichezo wa nchi mbalimbali, pia zilijaribiwa na kupokewa kwenye michezo ya XI ya Asia. Katika mashindano ya kwanza ya wushu ya kimataifa, njia hizo saba zilishindaniwa na pia kumekuwepo na vipimo vya kukadiria pointi.

Ingawa wushu ilianzia China lakini sasa ni kama urithi wa dunia. Tunaamini kuwa itakuwa kama ua jipya katika michezo ya ridhaa duniani.

picha husika>>

1  2