Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-11 19:20:20    
Sudan yafuata njia ya amani

cri
    Viongozi wa serikali ya umoja wa taifa wa Sudan waliapishwa tarehe 9 huko Khartoum. Mbali na rais Omar hassan El-Bashir na makamu wa rais wa serikali ya zamani kuwa rais na makamu wa pili wa rais, kiongozi wa chama cha ukombozi wa watu wa Sudan Bw. John Garang, ambaye aliongoza jeshi la kupinga serikali kusini mwa Sudan kwa miaka 22, amekuwa makamu wa kwanza wa rais. Alipotoa hotuba Bw. Garang alisema, "Leo nimeonekana hapa, hii inaonesha kuwa vita imekwisha, sasa amani imefika." Nchi ya Sudan hivi sasa imeingia kwenye njia ya amani.

    Sudan iko pembezoni mwa jangwa la Sahara, sehemu ya kaskazini mashariki ya bara la Afrika, nchi hiyo ina makabila mengi, migongano ya kikabila na kidini.

    Tarehe 1 mwezi Januari mwaka 1956, Sudan ilipata uhuru. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilitokea kati ya sehemu za kusini na kaskazini nchini Sudan kabla ya nchi hiyo kupata uhuru. Mwezi Machi mwaka 1972 serikali ya Sudan ilisaini mkataba wa kujiendesha kwenye sehemu ya kusini pamoja na wawakilishi wa sehemu ya kusini, vita ya kwanza nchini humo ikamalizika. Mwaka 1983 baadhi ya wanajeshi wakiongozwa na Garang walifanya uasi dhidi ya uamuzi wa serikali kutekeleza sheria ya kiislam kote nchini humo ndipo ikazuka vita ya pili kati ya sehemu za kaskazini na kusini.

    Vita vya wenyewe kwa wenyewe ni moja ya vita iliyodumu kwa miaka mingi barani Afrika, ambayo hadi hivi sasa imesababisha vifo vya watu milioni zaidi ya 2 na watu milioni zaidi ya 4 kukimbia makazi yao. Mapigano ya kijeshi na mgogoro wa kisiasa wa miaka mingi umefanya uchumi wa Sudan kukumbwa na pigo kubwa na kuwa moja ya nchi maskini kabisa duniani.

    "Serikali ya uokoaji imetimiza ahadi" hii ni bango linaloonekana siku hizi katika sehemu muhimu za Khartoum. Serikali ya uokoaji inayotajwa ni serikali inayoongozwa na Bashir, baada ya kushika madaraka mwezi Juni mwaka 1989, serikali hiyo ikachukulia utatuzi wa suala la sehemu ya kusini kuwa kazi yake muhimu kabisa.

    Makamu wa rais Ali Osman Taha, ambaye katika muda mrefu uliopita alikuwa kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Sudan katika mazungumzo ya amani, tarehe 9 alipotoa hotuba katika sherehe ya kuapishwa alisema kuwa pande mbili za kaskazini na kusini zinapofanya mazungumzo ya amani vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo inapamba moto, watu wenye msimamo mkali wa pande hizo mbili wote walipambana kufa na kupona wakinuia kulinda maslahi yao. Hata baada ya kuanza kwa mazungumzo ya amani, vita na mazungumzo viliendelea kwa wakati mmoja kwa miaka kadhaa. Alisema, "Amani inapatikana kwa shida kubwa", hayo ni matokeo yaliyopatikana kutokana na juhudi za pamoja za pande mbili zilizopambana na jumuiya ya kimataifa.

    Kutokana na usuluhishi wa Jumuiya ya maendeleo ya IGAD na Umoja wa Afrika, serikali ya Sudan na chama cha ukombozi wa watu wa Sudan zilifikia makubaliano huko Nairobi kuhusu masuala muhimu yakiwemo kujiamulia kwenye sehemu ya kusini, uhusiano kati ya dini na serikali na hifadhi ya umoja wa taifa na vilisaini mkataba wa amani tarehe 20 mwezi Julai mwaka 2002. Tarehe 31 mwezi Desemba mwaka jana pande mbili zilisaini nyaraka mbili za mwisho za mkataba wa amani, hatua ambayo ilimaanisha kufanikiwa kwa mazungumzo ya amani. Tarehe 9 Januari mwaka huu Bashir na Garang walisaini mkataba wa amani mjini Nairobi.

    Hivi sasa vikundi vidogo vya wanamgambo vinaendelea kufanya shughuli za uharibifu kwenye sehemu ya mashariki ya Sudan na kutishia utulivu wa huko isipokuwa bado hazijabadilika kuwa migogoro ya kijeshi. Sehemu ya mashariki ya Sudan kuna njia pekee ya kuendea baharini nchini Sudan ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo. Hivi sasa serikali ya Sudan imechukua hatua kutuliza hali ya huko.

    Wachambuzi wanaona kuwa kufikiwa mkataba wa amani kati ya sehemu za kaskazini na kusini na kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ni mwanzo mzuri wa mchakato wa amani nchini Sudan. Kutokana na juhudi zinazofanywa na pande mbalimbali husika, Sudan inakaribia zaidi na zaidi amani na hali ya utulivu.

Idhaa ya Kiswahili