Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Korea ya kaskazini jana alisema kuwa Korea ya kaskazini itajitahidi kuwania maendeleo halisi ya mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyukilia la peninsula ya Korea ya kaskazini. Siku moja kabla televisheni ya serikali kuu ya Korea ya kaskazini ilitangaza kuwa Korea ya kaskazini itarejea kwenye mazungumzo ya pande 6 mwishoni mwa mwezi Julai. Pande nyingine 5 zinazoshiriki mazungumzo ya pande 6 zilipongeza uamuzi huo wa Korea ya kaskazini.
Tarehe 9, naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea ya kaskazini Bw. Kim Kye-gwan alikuwa na mazungumzo na msaidizi wa waziri wa mambo ya nje anayeshughulikia mambo ya Asia ya mashariki na Pasifiki Bw. Christopher Hill mjini Beijing. Korea ya kaskazini ilitangaza kuwa katika mazungumzo hayo serikali ya Marekani imekiri kuwa Korea ya kaskazini ya nchi yenye mamlaka, na kusema kuwa Marekani haiwezi kuishambulia Korea ya kaskazini, na kuwa Marekani inakubali kushiriki kwenye mazungumzo ya pande mbili ndani ya mpango wa mazungumzo ya pande 6. Korea ya kaskazini inaona kuwa maneno hayo ya Marekani yanaweza kuchukuliwa kama ni kuondoa maneno iliyosema kuhusu "Korea ya kaskazini ni askari doria ya utawala wa kidhalimu, hivyo inaamua kurejea kwenye mazungumzo ya pande 6 mwishoni mwa mwezi Julai.
Rais Hu Jintao wa China jana alipokuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice ambaye hivi sasa anaitembelea China, alisema kuwa China inafurahia kufanyika upya kwa mazungumzo ya pande 6 na kupongeza pande zote husika kwa juhudi ilizofanya. Serikali ya Marekani pia inakaribisha Korea ya kaskazini kurejea kwenye mazungumzo ya pande 6 na kutarajia mazungumzo yatapata mafanikio. Korea ya kusini, Japan na Russia pia zinafurahia uamuzi wa Korea ya kaskazini.
Mgongano kati ka Korea ya kaskazini na Marekani ulikuwa mkali toka tarehe 10 mwezi Februari mwaka huu, ambapo Korea ya kaskazini ilitoa taarifa kusema kuwa na silaha za nyukilia na kutoshiriki mazungumzo ya pande 6.
Korea ya kaskazini inaitaka Marekani itambue kuwa Korea ya kaskazini ni nchi yenye mamlaka na kuondoa maneno iliyosema kuhusu Korea ya kaskazini ni doria ya utawala wa kidhalimu. Licha ya hayo, Korea ya kaskazini inataka kuwa na mazungumzo ya upunguza zana za kijeshi na Marekani kwa usawa. Marekani ilikataa kabisa na kutaka Korea ya kaskazini irejee kwenye mazungumzo ya pande 6 bila sharti lolote na kuacha kabisa mpango wa uendelezaji wa silaha za nyukilia. Mbali na hayo, Marekani iliitishia Korea ya kaskazini kwa kuwasilisha suala la nyukilia la peninsula ya Korea kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa na kuiwekea vikwazo vya kiuchumi, hatua ambayo ilifanya uitishaji wa mazungumzo ya pande 6 kuwa na utata mwingi.
Lakini pande mbili zilitambua haraka kuwa makabiliano hayo hayasaidii utatuzi wa matatizo na yataleta athari kwa pande zote mbili. Hivyo misimamo ya pande mbili ilianza kulegea.
Vyombo vya habari vinaona kuwa kwa vyovyote vile duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 litafanyika, kwa hivi sasa jambo muhimu ni namna ya kufanya mazungumzo hayo kupata maendeleo halisi. Watu wanatarajia pande mbili za Korea ya kaskazini na Marekani zitachukua msimamo wenye unyumbufu zaidi na kupiga hatua mbele halisi ili kuharakisha utatuzi wa suala la nyukilia la peninsula ya Korea.
Idhaa ya Kiswahili
|