Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-12 16:46:27    
Uamuzi wa Israeli wa kujenga ukuta wa utenganishaji wa Jerusalem ya mashariki waalumiwa

cri

Baraza la mawaziri la Israeli hivi karibuni liliamua kuharakisha ujenzi wa ukuta wa utenganishaji wa Jerusalem ya mashariki, uamuzi huo umelaumiwa na Palestina na jumuuia ya kimataifa.

Kutokana uamzi huo uliotolewa tarehe 10 kwenye baraza la mawaziri la Israel, Israeli itakamilisha ujenzi wa ukuta wa utenganishaji wa Jeusalem ya mashariki. Ukuta huo utapita sehemu ya wakazi wa Palestina ya Jerusalem ya mashariki, na kuwatenganisha wapalestina elfu 55 hivi wa Jerusalem ya mashariki nje ya ukuta huo na kuwa wakazi wa kando ya magharibi ya Mto Jordan. Katika miaka mingi iliyopita wapalestina hao waliishi ndani ya eneo la usimamizi wa serikali ya mji wa Jerusalem, walipewa kadi za kuishi kwa muda mrefu zilizotolewa na serikali ya Israel, na watu wengi kati yao wanafanya kazi, kusoma na kufanya biashara huko Jerusalem ya mashariki, na kupata huduma zilizotolewa na serikali ya Israel.

Ili kupunguza athari mbaya ya ujenzi wa ukuta wa utenganishaji kwa maisha ya wapalestina hao, serikali ya Israel imeamua pia kujenga njia 12 kwenye ukuta wa utenganishaji ili kuwarahisisha wapalestina hao waingie na kutoka Jerusalem ya mashariki, tena imeagiza idara mbalimbali za elimu na afya za Israel zichukue hatua za kuma mabasi kuwapeleka wanafunzi wa Palestina kupita ukuta wa utenganishaji kwenda Jerusalem ya mashariki kusoma shuleni, na kutoa huduma rahisi kwa wapalestina kwenda hospitali za Jerusalem ya mashariki. Serikali ya Israel pia imeahidi kuendelea kutoa huduma za jamii za bima na ajira kwa wapalestina hao.

Ingawa serikali ya Israel ilisema kuwa kujenga ukuta wa utenganishaji ni kwa ajili ya kuboresha mazingira ya usalama ya Israel, lakini kutokana na hali nyeti ya hadhi ya Jerusalem, vyombo vya habari vinaona kuwa, uamuzi huo wa Israel kabisa siyo kutokana na lengo la usalama tu. Waziri wa serikali ya Israel Haim Ramon tarehe 11 alikiri kuwa, mwelekeo wa ukuta wa utenganishaji wa sehemu zilizo pembezoni mwa Jerusalem utayaweka makazi makubwa zaidi ya wayahudi Maaleh Adumim yaliyoko magharibi ya Mto Jordan kwenye upande wa Israel, na kuwazuia wapalestina zaidi ya elfu 50 nje ya Jerusalem, lengo lake ni kuimarisha umaalum wa uyahudi wa Jerusalem, ili kuifanya Jerusalem kuwa mji mkuu wa kikweli wa Israel.

Ndiyo maana, mpango wa serikali ya Israel kuhusu ujenzi wa ukuta wa utenganishaji wa Jerusalm ya mashariki umelaumiwa na pande mbalimbali pamoja na Palestina. Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Abas tarehe 11 alisema kuwa, mpango huo wa Israel si kama tu hausaidii kuboresha usalama wa Israel yenyewe, bali pia hausaidii Palestiina na Israel kutimiza amani, kwa kweli ni kuweka vikwkazo kwa mchakato wa amani. Alisema, Palestina kamwe haiwezi kukubali ujenzi wa ukuta wa utenganishaji kwenye ardhi yake. Waziri mkuu wa serikali inayojiendesha ya Palestina Ahmed Qureia alisema kuwa, Iseral "inaiba ardhi ya Palestina kimachomacho", na kuchezesha mazungumzo ya amani. Hii itaufanya mpango wa upande mmoja wa Israel kuondoka Ghaza kuwa mpango usio na maana hata kidogo. Mwakilishi wa kwanza wa Palestina kwenye mazungumzo Bwana Saeb Erekat aliona kuwa, Israel inawazuia wapalestina nje ya Jerusalem kwa kusudi la kudhibiti vizuri zaidi Jerusalem, na kuamua peke yake umilikaji wa Jerusalem kabla ya kuanzisha mazungumzo kuhusu hadhi ya mwisho kati ya Palestina na Israel.

Msemaji wa Umoja wa nchi za kiarabu Hossam Zaki tarehe 11 huko Cairo alilaani uamuzi wa baraza la mawaziri la Israel akisema kuwa huu ni kitendo cha kudharau sheria ya kimtaifa. Alisisitiza kuwa Israel akikubali asikubali, Jerusalem daima itakuwa mji mkuu wa Palestina.

Mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya Javier Solana anayeitembelea Israel pia alisema kuwa, Umoja wa Ulaya inaona kuwa Israel ina haki ya kujilinda, lakini kujenga ukuta wa utenganishaji nje ya ardhi ya Israel, hii hailingani na sheria na italeta matatizo mengi ya kibinadamu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-12