Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-14 15:53:44    
China yaimarisha kazi ya kuingilia vitendo vyenye hatari kubwa ya kuambukiza ugonjwa wa ukimwi

cri

Kuanzia miaka 6 iliyopita, China ilianzisha kazi ya kuingilia kati ya vitendo vyenye hatari kubwa ya kuambukiza ugonjwa wa ukimwi katika sehemu kadhaa nchini. Kutumia sindano kwa pamoja kwa matuzi ya dawa za kulevya ni njia kuu ya kuambukizwa kwa ugonjwa wa ukimwi nchini China, hivyo China imechukua hatua za kutekeleza hatua ambayo kuwapatia watumiaji wa dawa za kulevya dawa ya Methadone badala ya matibabu, kuwataka watumie sindano safi na kuwataka wanawake wanaofanya kazi ya ukahaba watumie kondomu na kadhalika.

Matumizi ya dawa ya Methadone badala ya matibabu yalianzishwa mikoani Yunnan, Guangxi na Guangdong, kusini mwa China. Mtaalamu wa kinga na udhibiti wa ukimwi wa China Bwana Xu Jie akifahamisha alisema:

Matumizi ya dawa ya Methadone badala ya matibabu yalifanyiwa majaribio nchini China kuanzia mwaka 2004, wakati huo tulianzisha vituo vinane vya matibabu hayo, kila kituo kinawatibu watumiaji 200 hadi 300 wa dawa za kulevya. Kutokana na hali ya majaribio ya mwaka huu, tunaona matokeo yake ni mazuri.

Nchini China, kutokana na vyombo vya kudunga sindano ni bidhaa za matibabu, kwa kawaida vyombo hivyo haviuzwi katika maduka ya kawaida, hivyo watumiaji wengi wa dawa za kulevya hawawezi kupata vyombo hivyo na kulazimika kutumia sindano kwa pamoja. Ili kuwaepusha watumiaji hao wasiambukizwe virusi vya ukimwi kutokana na kutumia sindano kwa pamoja, mkoa wa Hunan wa katikati ya China na mikoa mingine imetekeleza hatua nyingine za kuingilia kati vitendo vya watumiaji wa dawa za kulevya, yaani inawapa bure sindano safi, hata watumiaji hao wanaweza kupewa sindano mpya safi kutokana na sindano walizowahi kuzitumia. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2004, vituo vya kutoa sindano safi vimezidi 50 nchini China.

Kuwataka wanawake wanaofanya kazi ya ukahaba watumie kondomu pia ni hatua moja ya China ya kuingilia vitendo vyenye hatari kubwa ya kuambukiza ugonjwa wa ukimwi. Kutokana na hali ya majaribio ya utekelezaji wa hatua hiyo katika mikoa mitano ya Hubei na Hunan, katikati ya China, zaidi ya asilimia 90 ya wanawake wanaofanya kazi ya ukahaba walitumia kondomu. Hivi sasa mikoa mingi ya China imeanzisha utekelezaji wa hatua hiyo.

Ili kukamilisha zaidi kazi ya kuingilia kati vitendo vyenye hatari kubwa ya kuambukiza ugonjwa wa ukimwi, hivi karibuni China imetoa "Mpango wa uelekezaji wa kazi ya kuingilia kati vitendo vyenye hatari kubwa ya kuambukiza ugonjwa", Bwana Xu Je wa kituo cha kinga na udhibiti wa maradhi cha China alisema, mpango huo umejumuisha kikamilifu kazi zilizofanyika katika siku zilizopita, na utazitumia sehemu mbalimbali kwa kuelekeza kazi zinazofanyika hivi sasa, ili kazi hiyo ipate mafanikio makubwa zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-14