Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-14 17:41:50    
Mji wa Changsha

cri

Mji wa Changsha ni mji mkuu wa mkoa wa Hunan, pia ni kituo cha kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, sanyasi, elimu na habari cha mkoa huo. Mji huo umewekwa kwenye orodha ya kwanza ya miji maarufu ya kihistoria na kiutamaduni na baraza la serikali ya China, na ni mmoja wa miji iliyofungua mlango mapema zaidi kwa nchi za nje. Eneo la mji huo ni kilomita za mraba 11.8 elfu, idadi ya watu ni milioni 6.018. Mji wa Changsha una mandhari nzuri na hali ya hewa ya kupendeza. Mjini humo kuna Mlima Yuelu na Mto Xiangjiang. Mji huo una historia ndefu, na watu wengi mashuhuri waliwahi kuishi kwenye mkoa huo. Hapo kuna kaburi la Mawangdui la Enzi la Han ambalo ni maarufu sana duniani, shule ya Yuelu yenye historia ya zaidi ya miaka elfu moja. Katika zama hizi wanasiasa, wanajeshi na wanafasihi wengi mashuhuri waliishi mjini humo.

Katika miaka zaidi ya 20 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, uchumi wa Mji wa Changshang ulipata maendeleo makubwa, sura ya mji huo ilibadilika siku hadi siku, na maisha ya wakazi yaliendelea kuboreshwa. Mwaka 2003, thamani ya uzalishaji(GDP) ya mji huo ilikuwa ni yuan za renminbi bilioni 92.822.

Sekta ya viwanda inapata maendeleo ya kasi. Hivi sasa kuna sehemu mbili za maendeleo ya uchumi za kitaifa mjini humo, yaani sehemu ya maendeleo ya teknolojia ya juu na kisasa ya Changsha na sehemu ya maendeleo ya teknolojia ya kiuchumi ya Changsha. Sekta za upashanaji habari wa elektroniki, utengenezaji wa mitambo, tumbaku, chakula, na dawa zimekuwa sekta muhimu mjini humo.

Mji wa Changsha ni kituo muhimu cha uzalishaji wa nafaka na ufugaji wa nguruwe. Aina mbalimbali za mazao ya kilimo yanazalishwa mjini humo, pamoja na samaki, mboga, matunda, maua, tumbaku, chai, na uyoga.

 

Biashara inastawi sana mjini humo. Wafanyabishara walianza kukusanyika huko tangu enzi na dahari. Mwishoni mwa enzi ya Qing, mji wa Changsha ulikuwa moja ya masoko manne ya michele nchini China. Hivi sasa majengo mengi ya kisasa ya bidhaa yamejengwa. Biashara mjini humo ina athari muhimu mkoani Hunan na hata nchini China. Sekta za chakula, utamaduni, utalii na biashara ya nyumba zina umaalumu wake wa kipekee, na sekta za benki, bima, hisa na biashara ya fedha za kigeni zinastawi siku hadi siku.

Kiwango cha maendeleo ya elimu na sayansi ni cha juu mjini Changsha. Hivi sasa kuna vyuo 37 vyenye wanafunzi laki 2.7, taasisi 97 za utafiti wa sayansi na wafanyakazi zaidi ya laki 2.7 wa utafiti wa sayansi. Teknolojia za mpunga chotara, kompyuta mkubwa ya aina ya milky way, utungaji mimba kwa njia isiyo ya asili, sayansi ya jeni, treni ya sumaku zote zimefikia kiwango cha juu duniani.

   

Hali ya mawasiliano ya mji wa Changsha ni nzuri, mfumo wa kisasa wa mawasiliano umeanzishwa. Na uwezo wa upashanaji habari wa mji huo unachukua nafasi ya tatu nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-14