Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-15 14:20:17    
Korea ya Kusini, Marekani na Japan zasawazisha misimamo kwa ajili ya duru jipya la mazungumzo ya pande sita

cri

Tarehe 14 wajumbe wa ngazi ya juu wa Korea ya Kusini, Marekani na Japan walifanya mazungumzo ya kusawazisha misimamo katika mji mkuu wa Korea ya Kusini, Seoul, kwa ajili ya duru la nne la mazungumzo ya pande sita yatakayofanyika hivi karibuni.

Tokea tarehe 10 Julai, Korea ya Kaskazini ilipotangaza kuwa itarejea tena kwenye mazungumzo ya pande sita, mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la penisula ya Korea ambayo yalikwama kwa zaidi ya mwaka mmoja, yametokewa na matumaini mapya. Pande zote zilionesha kukaribisha uamuzi huo wa Korea ya Kaskazini na kutumai kuwa duru jipya la mazungumzo hayo litapata matokeo ya maana. Katika mazingira hayo nchi hizo tatu zilifanya mkutano na kujadili lengo litakalofikiwa katika mazungumzo ya duru jipya na namna ya kufikia lengo hilo.

Kwenye mkutano, kimsingi Marekani ilishikilia msimamo wake uliotolewa katika mazungumzo yaliyopita, kwamba inaweza kuihakikishia Korea ya Kaskazini usalama, msaada wa nishati na kuondoa vikwazo pindi Korea ya Kaskazini "itakapoacha kabisa mpango wa nyuklia ambao unaweza kukaguliwa na isirudie tena". Katika mazungumzo yaliyopita, Korea ya Kaskazini ilishikilia "pande mbili zitende mambo kwa wakati mmoja", na vilevile ilitaka Marekani ikubali kutoa msaada wa nishati, kufuta Korea ya Kaskazini kutoka "orodha nyeusi ya magaidi" na kuacha kabisa uhasama kwa Korea ya Kaskazini. Lakini pande mbili hazikuafikiana.

Tarehe 12, Korea ya Kusini ilitangaza kuwa "Iwapo Korea ya Kaskazini itaahidi kuacha mpango wa nyuklia, Korea ya Kusini itaisaidia Korea ya Kaskazini nguvu za umeme kila mwaka" ili kutatua tofauti kati ya Korea ya Kaskaizni na Marekani. Korea ya Kusini iliahidi kuwa nchi hiyo itaanza kusaidia Korea ya Kaskazini kwa kuipatia umeme kuanzia mwaka 2008, na kabla ya mwaka huo itaisaidia mafuta mazito na gharama zitalipwa na nchi nyingine tano kwa kugawana.

Imefahamika kuwa kwenye mkutano huo wa pande tatu, ushauri huo wa Korea ya Kusini kuhusu namna ya kushirikiana na kupatana na msimamo wa Marekani ilijadiliwa sana. Wajumbe wa pande tatu wanaona kuwa pendekezo lililotolewa na Korea ya Kusini ni "ushauri mzito" ambao unasaidia utatuzi wa suala la nyuklia ya penisula la Korea.

Wajumbe wa pande tatu wanaona kuwa maduru matatu ya mazungumzo yaliyopita yote yalifanywa kwa aina ya "mkutano mkubwa", ajenda ilikuwa suala la nyuklia. Lakini matokeo yalikuwa kila upande ulishikilia msimamo wake na mazungumzo hayakuwa juu ya suala moja. Pande tatu zinaona kuwa inafaa kuunda vikundi au kamati ndogo ili kuandaa masuala halisi na kisha kuwasilisha kwenye mkutano mkubwa ili mazungumzo yawe na ufanisi.

Wafafanuzi wanaona kuwa maduru matatu ya mazungumzo yaliyopita yameweka jukwaa la mazungumzo. Tokea duru la kwanza ambapo kila upande ulieleza msimamo wake na kuweka kanuni hadi duru la pili ambapo pande zote zilianza kuzungumza masuala halisi na kufikia duru la tatu ambapo misimamo ya Korea ya Kaskazini na Marekani ilibadilika, kila duru lilipata maendeleo kwa kiasi fulani. Lakini kutokana na tofauti kubwa kati na Korea ya Kaskazini na Marekani na sababu nyingine, maduru matatu ya mazungumzo yaliyopita hayakupiga hatua kubwa.

Hivi sasa, kila upande unadai kuwa utajitahidi kufanikisha duru jipya la mazungumzo. Watu wamekuwa na matumai makubwa na duru jipya la mazungumzo baada ya kusubiri kwa muda mrefu, na wanatumai kuwa kila upande utachukua msimamo ulionyumbulika na kufanikisha mazungumzo hayo.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-15