Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-15 20:52:14    
Serikali ya Kenya yachukua hatua kutuliza hali ya sehemu ambako ulikotokea mgogoro wa kikabila

cri

Msemaji wa serikali ya Kenya Bw. Mutua tarehe 14 kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa, baada ya mgogoro wa kikabila kutokea huko Marsabit, serikali ya Kenya imechukua hatua nyingi kutuliza hali ya huko.

Bw. Mutua alisema kuwa, baada ya mgogoro huo kutokea, serikali ya Kenya ilituma jeshi na askari kwenda Marsabit mara moja, ili kulinda usalama wa huko. Hivi sasa polisi wanatafuta watu walioanzisha mgogoro huo. Wakati huo huo, serikali inashirikiana na idara ya uokoaji kupeleka chakula, dawa na vifaa vya matibabu katika sehemu hiyo. Aidha, serikali pia ilituma madaktari na wataalamu wa sakolojia, ili kuwapatia wakazi wa huko matibabu na huduma za kisakolojia.

Bw. Mutua alisema kuwa, serikali ya Kenya itaharakisha uchunguzi na kuwaadhibu watu wote waliioanzisha mgogoro huo. Alitoa mwito akiwataka watu wa makabila mbalimbali wawe watulivu, na wasianzishe mashambulizi ya kulipiza kisasi, ili kuzuia hali isizidi kuwa mbaya zaidi.

Tarehe 12 alfajiri katika sehemu ya Marsabit iliyoko kaskazini mwa Kenya, watu wenye silaha zaidi ya mia 3 kutoka kabila la Waborana walishambulia vijiji viwili vya kabila la Wagabra. Baadaye watu wa kabila la Gabra walishambulia gari la mtu wa kabila la Waborana. Watu wasiopungua 75 wakiwemo watoto 26 waliuawa, watu makumi kadhaa walijeruhiwa, na watu zaidi ya 6000 walikimbia makazi yao. Huu ni mgogoro mkubwa zaidi kutokea nchini Kenya katika miaka ya karibuni nchini Kenya.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-15