Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-15 21:07:53    
Tabia za wayi za kuvaa mapama

cri

Matawi mbalimbali ya kabila la Wayi, kila moja likiwa na desturi, mavazi na mila zake yanatapakaa huko na huko katika eneo pana la mikoa ya Yunnan, Guizhou na Sichuan. Mavazi yao, hasa ya wanawake yana uzuri wa kipekee na yanatofautiana sana na yale ya watu wa kabila la wahan waliowengi. Wanawake wa kabila hilo huyapa umakini mkubwa mapambo ya kichwani na ya nywele.

Wanawake wa kabila hilo wanaoishi kandokando ya Mto Jinsha (sehemu moja ya juu ya Mto Changjiang) katika mlima Daliang na mlima Xiaoliang, huvaa kichwani vitambaa vilivyotariziwa ambavyo hutelemka hadi kwenye sehemu ya kati ya paji la uso; nywele zao zilizosukwa katika mikufu miwili hubanwa juu kwa pini nyeupe na ndefu. Vipande virefu na vyeupe vya majohari hutundikwa juu ya vitambaa hivyo na kuachwa vining'inie chini ya masikio yao vikileta tofauti kubwa baina ya mapambo hayo na sketi ndefu nyeusi za wanawake hao.

Wanawake wa kabila la wayi wa mkoa wa Guizhou pia huvaa vitambaa vyenye tarizi vichwani, na kwa kawaida huwa wakitundika vishada vya nyuzi na ushanga kwenye sehemu ya mbele ya paji la uso. Mabegani mwao hujitanda mtandio wenye mabombwe yliyofumwa.

Wanawake wa kabila la wayi wanaoishi katika maeneo ya Mto Honghe, mkoa wa Yunnan, wana mtindo wao wenyewe wa vilemba. Wao huvaa skafu nyeusi zilizotarizwa maua na kupambwa kwa mikufu ya fedha yenye kishada cha nyuzi katika kila ncha ambavyo huning'inia mabegani. Pia huvaa hereni kubwa. Baadhi ya wanawake wa maeneo hayo huvaa pambo la kichwani lenye umbo la upanga wa jogoo lililopambwa kwa mikufu ya fedha, vifungo na ushanga, vitu ambavyo hung'ara katika mwanga wa jua. Inasemekana kuwa, "taji" kama hilo hugharimu kiasi cha yuan 1,000 na huwa ni sehemu ya mahari ya wasichana wa kabila la wayi.

Kuna matawi 13 madogomadogo ya Wayi huko Chuxiong, mkoani Yunnanm ambao wengi wao huishi katika maeneo ya milimani, wanawake wa Yuanmou huvaa mapama yaliyotengenezwa kwa sufu nyekundu ambayo huonekana kama mipira mikubwa ya manyoya laini; kwenye pande zote mbili hufungwa mashada ya nyuzi nyeusi za sufu ambazo hufika hadi mabegani. Wakati mwingine wanawake husokota ukambaa wa sufu nyekundu?ambao unaweza kuwa na uzito wa kilo nne hivi na kuunyonganyonga kichwani na kuacha ncha yake moja ikining'inia juu ya bega la kushoto. Wanawake wa Lufeng huvaa mapama laini yaliyotarizwa na kufumwa kwa mfumo wa kuhesabu, na kwenye ukingo, mapama hayo hupambwa kwa kome na kengele ndogondogo za fedha ambazo hutoa mlio. Wakati wa sherehe, mchezaji kiongozi wa ngoma mara nyingi huvaa pama la jingling.

picha husika>>

1  2