Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-18 16:48:26    
Sehemu ya Taohuayuan yenye vivutio vya mandhari mkoani Hunan, katikati ya China

cri

Sehemu ya Taohuayuan iko katika Wilaya ya Taoyuan mkoani Hunan. Mshairi maarufu wa China ya kale Tao Qian aliwahi kuandika insha moja ya kusimulia kijiji kimoja cha sehemu hiyo. Katika insha yake alisema, kijiji hicho kidogo kimejificha ndani ya milima ya mbali, kwenye sehemu ya chanzo cha kijito ambacho kingo zake mbili kuna miti mingi ya maua ya Taohua yaani maua ya peoni, kijiji hicho kina mandhari nzuri sana tena kiko mbali na sehemu nyingine, na hakijawahi kukumbwa na vurugu za vita hata mara moja, hivyo ni sehemu moja yenye usalama, utulivu na maisha mazuri. Kutokana na insha yake hiyo, wachina huichukulia sehemu isiyoathiriwa na nje au dunia yenye maisha mazuri kama waliyotarajia ndotoni kuwa ni sehemu ya Taohuayuan.

Insha hiyo iliandikwa zaidi ya miaka 1600 iliyopita, lakini siku zote inasomwa na wachina, mpaka sasa insha hiyo inawekwa kwenye kitabu cha mafunzo ya lugha ya kichina katika shule za sekondari. Ndiyo maana, sehemu ya Taohuayuan mpaka sasa bado inawavutia watu wengi kwenda huko kutafuta vivutio vya kale.

Hivi sasa sehemu ya Taohuayua imewekwa kuwa sehemu moja yenye vivutio inayosimamiwa, lakini vivutio vya sehemu hiyo vinaonekana ni vizuri vilevile kama alivyosimulia mwandishi wa kale Tao Qian katika insha yake, milima mirefu, mito yenye maji safi na miti mingi ya kale, ambapo pia kuna maua ya aina mbalimbali, ngazi ya mawe, vibanda vidogo vilivyotapakaa huku na huko. Wakati maua ya peoni yanapochanua, mandhari ya sehemu hiyo inapendeza sana.

Bwana Wang Junhui wa ofisi ya usimamizi wa sehemu hiyo alijulisha kuwa, sehemu hiyo yenye eneo la kilomita16 za mraba, kila mwaka inawavuta watalii wengi wa nchini na ng'ambo. Alisema:

Watalii hufikia laki 5.4 kila mwaka, miongoni mwao watalii kutoka nje hufikia elfu 20 hadi 30, na miezi ya Machi, Aprili, Mei, Septemba, Oktoba na Novemba ni kipindi kinachowavutia watalii wengi zaidi kwenye sehemu ya Taohuayuan.

Mbali na vivutio vya mandhari, sehemu ya Taohuayuan kuna chai Lei ambayo ni chai maarufu sana ya sehemu hiyo. Chai hiyo inatengenezwa kwa njia maalum kwa tangawizi, mchele na chai zisizopikwa. Inapotengezwa, kwanza mchele hukaangwa, halafu vitu vingine hukurogwa, kumimina maji ili kuufanya mchele uvimbe, halafu kukoroga na kuutwaga uwe uji, halafu kumimina maji baridi ndani ya uji, baadaye kutia maji yanayochemka, na kuwa chai ya Lei inayojulikana ya sehemu ya Taohuayua.

Mhudumu wa mkahawa wa chai Dada Wu Yanyan alimwambia mwandishi wa habari kuwa, kutokana na kumbukumbu ya historia, historia ya wenyeji wa huko kutengeneza chai ya lei imekuwa ya zaidi ya miaka elfu 10, hivi saa chai ya lei imekuwa kinywaji kisichokosekana katika maisha ya wenyeji wa huko. Alisema:

Chai ya lei ni kinywaji kizuri sana, hivyo kimedumishwa kizazi baada ya kizazi, wenyeji wa hivi sasa wanapotengeneza chai hiyo wanaongeza vitu vingi kama vile karanga, ufuta, soya na unga wa michele, wenyeji wanapokunywa chai hiyo hula pamoja na vitoweo vingine vya mboga za huko wanazopenda, hivyo kila wakisherehekea mwaka mmoja wa mtoto mchanga, hutengeneza chai hiyo pamoja na vitoweo vingi.

Na chai ya lei pia ni zawadi nzuri wanayozawadia wageni. Ukienda sehemu ya Taohuayuan, ukiingia kwenye kila familia, mwenyeji huweza kukukirimu kwa chai ya lei yenye ladha ya aina mbalimbali.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-18