Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Iraq Ibrahim al Jaafari tarehe 18 alimaliza zaria yake rasmi ya siku 3 nchini Iran. Hayo ni mawasiliano ya kidiplomasia ya ngazi ya juu kabisa kati ya Iran na Iraq tokea vita vya Iran na Iraq vifanyike. Vyombo vya habari vinaona kuwa ziara hiyo ya Jaafari imefungua ukurasa mpya wa historia ya uhusiano wa nchi hizo mbili.
Ikiwa nchi majirani, kuna mambo mengi ya namna moja kati ya Iran na Iraq, na nchi hizo mbili zote zina waislamu wengi zaidi wa madhehebu ya Shia. Lakini mwaka 1980, vita vilianzishwa kati ya nchi hizo majirani kutokana na mgogoro wa suala la mipaka, vita hivyo vilivyodumu kwa miaka minane vilisababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja, na nchi hizo majirani zikawa nchi zinazopambana. Miaka mingi imepita, na yaliyopita yamepita, tena aliyezusha vita hivyo Saddam Hussein wa utawala wa Iraq alipinduliwa, na kikwazo kikubwa kilichokwamisha maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili kimeondolewa. Hali ya hivi sasa imesaidia kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na maendeleo hayo ya uhusiano kati yao yamekuwa ya lazima kwa nchi hizo mbili.
Kwa Iran, nchi hiyo inatishiwa mara kwa mara na vikwazo vya Marekani kutokana na suala la nyuklia la Iran. Marekani inailaani mara kwa mara kuwa imewahifadhi wanachama wa "kundi la al Qaida" nchini humo au kuwaruhusu watu hao waingie Iraq kupitia Iran kufanya shughuli za kigaidi. Na uhusiano kati ya Iran na nchi kadhaa za kiarabu pia ulikuwa katika hali ya wasiwasi siku zote. Ndiyo maana, Iran inapaswa kuboresha kwanza uhusiano na Iraq ili kuboresha uhusiano kati yake na nchi zote za kiarabu zilizo za majirani yake. Mazingira ya pembezoni yaliyo ya utulivu na usalama yanaisaidia sana Iran, ambayo yataweza kuvunja hali ya upweke wa kidiplomasia iliyowekwa na Marekani. Zaidi ya hayo, fursa kubwa ya biashara kutokana na ukarabati wa Iraq pia ni fursa inayotarajiaw na Iran.
Kwa kuwa serikali ya mpito ya Iraq inayoongozwa na Bwana Jaafari ambayo imeshika madaraka kuanzia tarehe 1 Aprili, namna ya kuboresha hali ya usalama ya nchini Iran, kuzuia magaidi kuvuka mpaka kufanya shughuli za mashambulizi, kuendeleza uchumi udhaifu na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi, hayo ni mambo ya dharura kwa Iraq. Serikali ya Jaafari inaona kuwa, kuendeleza uhusiano mzuri na nchi jirani hasa Iran ni sharti la kwanza kwa maendeleo ya siasa na uchumi ya Iraq, hasa ni muhimu zaidi kwa hali ya usalama ya Iraq.
Wakati wa ziara hiyo, Bwana Jaafari na kiongozi wa Iran walieleza matumaini ya dharura ya kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili. Kuhusu vita vile vilivyosababisha hali wasiwasi ya muda mrefu kati ya nchi hizo mbili, Bwana Jaafari alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Iran tarehe 16 alisema kuwa, jukumu lake la safari yake ni kuondoa uelewa mbaya kati ya nchi hizo mbili kutokana na historia, na kuanzisha ushirikiano mpya katika sekta za siasa na uchumi.
Rais Khatami wa Iran tarehe 17 alipokutana na Bwana Jaafari alisema kuwa, ziara ya Jaafari nchini Iran itafuangua ukurasa mpya wa historia ya uhusiano wa Iran na Iraq. Wakati wa ziara ya Jaafari, Iran na Iraq zimeanza kuchukua hatua halisi za kuimarisha uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Idhaa ya Kiswahili 2005-07-19
|