Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-19 17:47:42    
Je "Shirikisho la nchi 4" na "Umoja wa Afrika" zinaweza kushirikiana au la?

cri

"Shirikisho la nchi 4" la Japan, India, Ujerumani na Brazil na Umoja wa Afrika tarehe 17 alasiri zilifanya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje huko New York, lakini hazikuweza kufikia makubaliano yoyote kuhusu upanuzi wa baraza la usalama. Uwezekano wa pande hizo mbili kushirikiana au la, ni jambo linalofuatiliwa sana na nchi husika.

Hivi sasa "Shirikisho la nchi 4" na Umoja wa Afrika zote zimekabidhi miswada yao ya azimio kuhusu upanuzi wa baraza la usalama, na yaliyomo kwenye miswada ya pande hizo mbili yanakaribiana sana, yaani zote zinataka kuongeza wajumbe wa kudumu na wasio wa kudumu kwenye baraza la usalama, tofauti ni kuwa, "Shirikisho la nchi 4" linataka kuongezeka kwa wajumbe 10, na Umoja wa Afrika unataka kuongezeka kwa wajumbe 11. Ili kuifanya miswada yao ipate kura zaidi ya theluthi mbili na kupitishwa kwenye Umoja wa Mataifa, pande hizo mbili zimeamua kushirikiana. Hali ya hivi sasa inaonesha kuwa, pande hizo mbili zikitaka kuondoa migongano na kushirikiana kuhusu suala hilo, bado zinakabiliwa na taabu nyingi.

Hivi sasa mgongano mkubwa zaidi kati ya pande hizo mbili ni kuwa, nchi wajumbe wapya wangepata haki ya kupiga kura ya turufu kama nchi wajumbe wa kudumu wa sasa zilivyofanya kwenye baraza la usalama. Haki ya kupiga kura ya turufu kwa nchi wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama inaonesha hali ilivyokuwa ya muundo wa dunia wakati vita vikuu ya pili ya dunia ilipomalizika, hii ni haki maalum ya kisiasa duniani iliyotokana na historia. Hivi sasa nchi hizo zinazotaka kuongezeka kwa wajumbe wa kudumu, kila moja inatarajia kupewa haki hiyo, lakini mbinu zao ni tofauti. Mwanzoni "shirikisho la nchi nne" lilieleza wazi kutaka kuwa na haki ya kupiga kura ya turufu, baadaye liliona kuwa huenda litalaumiwa na nchi nyingine kutokana na sababu hiyo, hivyo liliacha kwa muda dai hilo, na kuchukua mbinu za kupiga hatua mbili za kuwa wajumbe na kujipatia haki ya kupiga kura ya turufu. Nchi za Umoja wa Afrika zimeeleza wazi na kusisitiza kuwa lazima kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zinapata nafasi ya wajumbe wa baraza la usalama, na baada ya kuwa wajumbe wa kudumu lazima kuwa na haki ya kupiga kura ya turufu. Wachambuzi wanaona kuwa, hii imeonesha malalamiko ya nchi za Afrika ambazo kwa muda mrefu uliopita ziliwekwa nje ya sauti kuu ya jukwaa la kisiasa la dunia.

Aidha, hivi sasa "Shirikisho la nchi nne" linataka kuongezwa kwa nchi 4 za wajumbe wasio wa kudumu, nchi moja kati yao ingekuwa nchi ya Afrika, lakini Umoja wa Afrika unashikilia kuongeza nchi 5 wajumbe wasio wa kudumu, nchi mbili kati yao zingekuwa nchi za Afrika. Kuhusu suala hilo, nchi za Afrika zinasisitiza kuwa, ikiliganishwa na nchi 3 wajumbe wa kudumu wa bara la Ulaya, dai hilo la Afrika ni la kikomo cha chini. Mwakilishi wa kudumu wa Nigeria kwenye Umoja wa Mataifa alipofahamisha mswada wa azimio la Umoja wa Afrika alisema kuwa, wanaotaka kufanya mazugumzo na Umoja wa Afrika, wangeona ukweli wa mambo ambayo hakuna ujumbe wa kudumu wa nchi za Afrika kwenye baraza la usalama. Mwakilishi wa kudumu wa Misri katika Umoja wa Mataifa pia alidhihirisha kuwa, masuala ya Afrika yanachukua zaidi ya asilimia 60 kwenye ajenda za kawaida za baraza la usalama, lakini kutokana na historia na sababu nyingine, nchi za Afrika siku zote hazina ujumbe wa kudumu kwenye baraza la usalama.

Habari zinasema kuwa, mawaziri wa mambo ya nje wa Shirikisho la nchi 4 na nchi za Umoja wa Afrika watakutana tena tarehe 25 huko Geneva, wakati huo huo wawakilishi wa kudumu wa nchi hizo katika Umoja wa Mataifa wataendelea na mazungumzo. Lakini kama alivyosema waziri wa mambo ya nje wa India,  hivi sasa pande hizo mbili zinataka kupunguza migongano wala siyo kuondoa migongano. Hii inamaanisha kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili hayatakuwa rahisi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-19