Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-19 20:30:21    
Ushirikiano kati ya mashirika mbalimbali wasukuma mbele maendeleo ya uchumi wa mkoa wa Hunan

cri

Kijografia, Mkoa wa Hunan uko katika sehemu nzuri kwa kupakana na mtu wa kwanza kwa urefu nchini pamoja na mkoa wa Guangdong ambao ni mkoa ulioendelea sana kwenye pwani ya kusini ya China, lakini katika miaka mingi iliyopita, mkoa wa Hunan ulijulikana kwa mkoa mkubwa wa kilimo. Pato la mkoa huo liko nyuma ya nafazi ya zaidi ya 10 miongoni mwa mikoa zaidi ya 30 ya China, na jumla ya thamani ya mali ya viwanda, pato kutokana na maujzo ya bidhaa na faida liko katika nafasi ya kiasi cha 20. ili kuharakisha maendeleo ya uchumi, mkoa wa Hunan uliweka lengo la licha ya kutuliza uzalishaji wa chakula, utahimiza ujenzi wa viwanda na miji na kubadilisha mtindo wa ongezeko la uchumi. Mkuu wa mkoa wa Hunan Bw. Zhou Bohua alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema,

"Hunan ukiwa mkoa mkubwa wa kilimo na wenye idadi kubwa ya watu, ukitaka kuingia kundi la mikoa yenye nguvu kubwa ya kiuchumi hauna budi kuhimiza uzalishaji wa chakula wa kisasa na kuhimiza ujenzi wa miji kwa kutegemea nguvu imara ya viwanda."

Katika njia yake ya maendeleo ya viwanda, suala la kwanza linaloukabili mkoa wa Hunan ni namna ya kubadilisha mtindo wa viwanda wa jadi uliopitwa na wakati. Miongoni mwa viwanda maelfu kadhaa mkoni Hunan, vile vikubwa na wastani havijafikia theluthi moja. Hali hiyo duni ni dhahiri zaidi katika mazingira ya ushindani wa viwanda vya kisasa. Dhidi ya hali hiyo, Hunan ina wazo la kuunganisha viwanda hivyo ili kuvifanya visaidiane na kuleta maendeleo kwa pamoja. Kutokana na wazo hilo, Hunan ilianzisha kampuni ya viwanda vya mitambo katika Changsha, mji mkuu wa mkoa huo, ambayo ilinunua kampuni ya jadi ya mitambo ya uhandisi (engineering) ya Puyuan. Kampuni ya Puyuan ina uwezo mkubwa wa uzalishaji lakini teknolojia yake imepitwa na wakati, mwaka 2002 kampuni ya Puyuan ambayo hususan ilizalisha winchi, pato lake kutokana na mauzo lilikuwa Yuan milioni 800 na faida ilikuwa Yuan milioni kadhaa tu. Lakini hali ya kampuni ya Zhonglian iliyoanzishwa na taasisi ya utafiti wa mitambo ya ujenzi ya Changsha ni kinyume chake, ingawa ilikuwa na nguvu kubwa ya utafiti, pato lake kutokana na mauzo lilikuwa Yuan milioni 600 mwaka 2002 na kupata faida Yuan milioni 200, ingawa bidhaa zake zinauzwa sana, lakini uwezo wake haukuwa mkubwa, hivyo maendeleo ya kampuni yalizuiliwa.

Kampuni ya Zhonglian na kampuni ya Puyuan kila moja ilikuwa na hali yake bora na mahitaji yake, ambayo iliweke msingi wa kuungana pamoja. Naibu meya wa mji wa Changsha Bw. Liu Xiaoming alisema,

"Kampuni hizo mbili, kila moja ina hali yake bora na upungufu wake pia, baada ya kampuni hizo mbili kungana pamoja, nguvu yake ni kubwa zaidi kuliko hapo awali."

Naibu meya Liu alisema kuwa kuungana kwa kampuni hizo mbili kulikuwa jambo moja kubwa wakati ule katika sekta ya mitambo ya uhandisi. Baada ya kuunganishwa, kampuni ya Puyuan ilipata uungaji mkono wa mitaji na teknolojia kutoka kampuni ya Zhonglian. Faida iliyopata Puyuan mwaka 2004 ilizidi jumla ya faida ilizopata katika miaka 15 iliyopita kabla ya hapo. Kampuni ya Zhonglian iliimarishwa uwezo wake wa uzalishaji na pato kutokana na mauzo katika mwaka jana lilizidi Yuan bilioni 4.5. Kampuni hizo mbili zote zilifaidika.

Kuhimiza viwanda vyenye nguvu kungana pamoja ni moja ya hatua iliyochukuliwa na mkoa wa Hunan katika kubadilisha muundo wa uchumi, mbali na hayo, mkoa wa Hunan ilivutia wawekezaji wa nchi za nje kwa viwanda vyake bora ili kuhimiza viwanda vya mkoa vifanye ushirikiano na makampuni ya kimataifa na kuleta maendeleo ya kasi.

Trehe 1 mwezi Desemba mwaka 2004, kampuni ya Zhongqi ya Hunan ilisaini mkataba pamoja na kampuni kubwa kabisa duniani ya zana za magari ya Bosch ya Ujerumani. Kampuni ya Bosch ilinunua workshop mbili za injin na genereta za kampuni ya Zhongqi, ambapo kampuni ya Zhongqi ikawa mfanya biashara anayezalisha vipuri vya magari kwa ajili ya kampuni ya Bosch, pande hizo mbili zikaanzisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Zhongqi Bw. Zhang Guocai alisema kuwa hadi mwaka 2010, shighuli za kuzalisha vipuri vya magari kwa ajili ya Bosch zitaleta pato la Yuan bilioni 1.2 kwa mwaka. Bw. Zhang alisema,

"Teknolojia yetu ya uzalishaji vipuri inatokana na Bosch, endapo Bosch siyo mwenzetu bali ni mshindani watu, kwa uhakika hatutaiweza. Pamoja na kuimarika kwa nguvu ya Bosch nchini China, na kuichukulia China kuwa mfanya biashara wa kwanza duniani wa kuitosheleza vipuri, ninaona kuwa kampuni ya Zhongqi itakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kujiimarisha na kwa haraka zaidi."

Katika mahojiano, mwandishi wetu wa habari alifahamu kuwa idara husika za mkoa wa Hunan zilifanya kazi muhimu katika kuhimiza ushirikiano kati ya kampuni ya Zhongqi na Bosch, kutokana na uhimizaji wa idara za serikali, kampuni ya Zhongqi ilichukua mali zake bora kuvutia wawekezaji wa kigeni.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-19