Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-20 15:59:06    
Mapishi ya kupika matango machungu na nyama ya nguruwe iliyokaushwa

cri

Mahitaji

matango machungu gramu 300, nyama ya nguruwe iliyokaushwa gramu 150, vipande vya tangawizi, vitunguu saumu kila kimoja gramu 15, pilipili hoho gramu 10, mvinyo wa kupikia gramu 10, pilipili manga gramu 10, maji ya wanga gramu 10, chumvi na M.S.G kila kimoja gramu 5.

Njia

1. Kata nyama ya nguruwe iliyokashwa iwe vipande vipande na uviweke kwenye bakuli moja lenye maji kwa dakika 15. Pasua matango machungu na ondoa mbegu ndani ya matango machungu, na uyaoshe, halafu kata matango machungu yawe vipande.

2. tia mafuta kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe rangi ya nyuzi 50, tia vipande vya tangawizi, vitunguu saumu na pilipili hoho, koroga koroga, halafu tia vipande nyama ya nguruwe iliyokaushwa, korogakoroga na mimina mvinyo wa kupikia, tia vipande vya matango machungu, pilipili manga, chumvi na M.S.G, mimina maji kidogo, korogakoroga, tia maji ya wanga, korogakoroga, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa na kinafaa kuliwa wakati wa majira ya joto.