Kuanzia leo, China na nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki zinapunguziana hatua kwa hatua ushuru wa forodha wa bidhaa asilia aina 7000 za mwenzio. Hatua hii inamaanisha kuwa eneo la biashara huria kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki kuingia katika kipindi halisi ya ujenzi.
Khatua hiyo ya kupunguziana ushuru wa forodka kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki ilifikiwa mwaka jana na pande hizo mbili kutokana na kusainiwa "mkataba wa biashara ya bidhaa". Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Zong Quan alisema, "Mpango wa upunguzaji wa ushuru wa biashara ya bidhaa kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki ulizinduliwa rasmi tarehe 20 mwezi Julai, China na nchi 6 za Brunei, Indonesia, Malasia, Bumar, Singapore na Thailand za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki zinafuata kiasi cha utozaji ushuru wa eneo la biashara husia kati yao, ambapo nchi za Kampucha, Laos, Philippines na Vietnam zitatekeleza kiasi hicho cha ushuru pamoja na China baada ya nchi hizo kukamilisha mchakato wa uidhinishaji nchini mwao."
Kutokana na mkataba wa biashara uliofikiwa na China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki kuhusu biashara huria, nchi hizo zitapunguza hatua kwa hatua ushuru wa forodha wa aina 7,000 za bidhaa asilia za mwenzio ifikapo mwaka 2010 China na nchi wanachama 6 wa zamani yaani Brunei, Indonesia, Malasia, Bumar, Singapore na Thailand zitapunguza ushuru wa forodha karibu aina zote za aina hizo 7,000. Ifikapo mwaka 2015 ushuru wa bidhaa karibu aina zote kati ya China na nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki utapungua hadi sifuri.
Kuzinduliwa mpango wa upunguzaji ushuru kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki kunamaanisha kuwa eneo la biashara huria kati ya pande hizo mbili limeingia kipindi halisi cha ujenzi. Eneo la biashara huria linalojengwa hivi sasa kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki ni eneo la kwanza la biashara huria kati ya China na nchi nyingine, ambalo baada ya kukamilishwa ujenzi wake mwaka 2010 eneo hilo litakuwa na idadi ya watu bilioni 1.8 na thamani ya biashara ya eneo hilo itafikia dola za kimarekani trioni 2, ambalo licha ya kuwa eneo la kwanza kwa ukubwa katika bara la Asia, bali pia kati ya nchi zinazoendelea.
Mtafiti wa idara ya utafiti wa uchumi na siasa wa kimataifa ya taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Shen Jiru alifanya uchambuzi kuwa uchumi wa China na wa nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki una uwezo mkubwa wa kutoshelezana mahitaji ya mwenzio, kupunguziana ushuru wa forodha hadi kujenga eneo la biashara huria hatimaye kutaharakisha maendeleo ya uchumi ya pande hizo mbili. Alisema, "Kuzinduliwa mpango wa upunguzaji wa ushuru wa forodha kunamaanisha kuwa bidhaa zinaweza kuingiliana bila vipingamizi katika masomo mawili ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki, na pande zote mbili zitaimarisha nguvu ya ushindani ya bidhaa zake zenye hali bora. Hivyo ufanisi wa uzalishaji utainuliwa na rasilimali pia zitatumika ipasavyo."
Habari zinasema kuwa baada ya kupunguziana ushuru wa forodha kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki, usafirishaji wa bidhaa zenye hali bora za nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki zikiwemo mafuta ya asili ya petroli, gesi ya asili, mawese, mpira na mbao utaongezeka zaidi, wakati bidhaa za vyombo vya umeme vya nyumbani na nguo za China pia zitaweza kuingia masoko ya nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki bila vipingamizi, jambo ambalo litahamasisha maendeleo ya biashara ya nje ya pande hizo mbili.
Idhaa ya Kiswahili
|