Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-20 21:36:23    
Mashirika ya software ya Dalian yazingatia kuinua uwezo wa uvumbuzi kwa kujitegemea

cri

Mji wa Dalin ni mji wa pwani ulioko mkoani Liaoning, kaskazini mashariki mwa China. Katika miaka ya karibuni, sekta ya software ya mji huo imeendelea kwa kasi, na kuwa kituo muhimu cha sekta hiyo nchini China. Jambo muhimu katika kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya software ni kuwa na bidhaa zenye hakimiliki ya kujitegemea, hivyo mashirika ya software ya Dalian yanazingatia sana kuinua uwezo wa uvumbuzi kwa kujitegemea.

Sekta ya software ni sekta yenye mustakabali mzuri, katika miaka ya karibuni, sekta hiyo imeendelea kwa kasi kote duniani, na hatua kwa hatua imekuwa roho na msingi wa sekta ya upashanaji habari wa kisasa badala ya sekta ya hardware. Takwimu zinaonesha kuwa, thamani ya biashara ya software duniani katika mwaka jana ilifikia dola za kimarekani bilioni 880, ikiwa imeongezeka kwa asilimia 11 kuliko mwaka juzi. Sekta ya software ya China iko nyuma kidogo kimaendeleo duniani, na ilichukua asilimia 3 tu katika sekta hiyo duniani katika mwaka 2004.

Sehemu ya software ya Dalian iliyoko kwenye upande wa kusini ya mji huo, ina mashirika 250. miaka 7 tangu kuanzishwa kwa sehemu hiyo, thamani ya biashara imeendelea kuongezeka kwa asilimia 30 kila mwaka, na katika mwaka 2004, sehemu hiyo ilitimiza mapato zaidi ya yuan bilioni 3. Kuendelea kuinua uwezo wa uvumbuzi kwa kujitegemea ni jambo muhimu linalosukuma mbele maendeleo ya kasi ya sehemu hiyo.

Katika mchakato wa kuinua uwezo wa uvumbuzi kwa kujitegemea, suala la kwanza ni watu wenye utaalamu. Hivyo, mwaka 2001, sehemu hiyo ilishirikiana na mashirika husika na kujenga chuo cha teknolojia za upashanaji wa habari cha Dong Ruan, ambacho ni chuo kikubwa kabisa cha teknolojia ya software nchini China. Hivi sasa, chuo hicho kimekuwa chuo cha elimu ya juu chenye wanafunzi 9000 kinachoweza kutoa shahada ya kwanza, ya pili na ya tatu. Baadaye, sehemu hiyo ilijenga vyuo vitatu vya software. Aidha, kutokana na kuungwa mkono na serikali ya mji wa Dalian, vyuo vikuu 22 vilivyoko mjini humo vyote vimeanzisha elimu ya utaalamu wa software. Hali hiyo imeandaa watu wengi zaidi wenye utaalamu mbalimbali kwenye sehemu hiyo. Aidha, sehemu ya software ya Dalian pia ilitekeleza sera nyingi za kuwavutia wataalamu kutoka sehemu nyingine au nchi za nje kuanzisha shughuli zao mjini Dalian. Mkuu wa idara ya sekta ya upashanaji wa habari ya Dalian Bw. Luan Qingwei alieleza:

"kutokana na hali ya Dalian, ingawa mfumo kamili wa elimu mbalimbali husika umejengeka, lakini bado haitoshi, hivyo inapaswa kuwavutia na kuwaingiza wataalamu wa teknolojia za upashanaji wa habari kutoka sehemu mbalimbali nchini China na duniani kuja Dalian kuanzisha shughuli zao."

Mpaka sasa, sehemu hiyo ina wahandisi wa software 12,000, wengi miongoni mwao waliwahi kufanya kazi nchi za nje. Wataalamu hao wametoa msingi thabiti wa utaalamu kwa uvumbuzi wa kujitegemea wa mashirika hayo. Kama vile, shirika la teknolojia za kitarakimu la Comgi lilianzishwa kwa pamoja na baadhi ya maprofesa wa vyuo vikuu vya huko na wamarekani wawili wenye asili ya China. Maneja mkuu ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa shirika hilo Bw. Su Zhixun alieleza:

"Shirika hilo linasanifu software zenye hakimiliki. Nilifanya utafiti kuhusu picha za skrini za kompyuta kwa miaka zaidi ya kumi, hivyo nimekuwa uzoefu mkubwa katika eneo hilo. Washiriki wageni wawili wote ni wataalamu katika eneo hilo. Hivyo, lengo letu la kuanzisha shirika hilo ni kuendeleza bidhaa kwa kutegemea uzoefu wetu wenyewe wa utafiti wa miaka mingi. Tulichagua mji wa Dalian kwa kuwa mji huo una raslimali nyingi ya nguvu kazi na msingi mkubwa wa utafiti."

Mbali na kuandaa na kuwaingiza wataalamu, katika miaka ya hivi karibuni, mashirika yaliyoko kwenye sehemu hiyo pia yanafanya juhudi kuinua kiwango cha utafiti kwa kutumia fursa ya mashirika ya kigeni kuhamia kwenye sehemu ya huduma ya upashanaji wa habari kwenye kanda ya Asia na Pasifiki. Hivi sasa, kutokana na kuwa gharama za uzalishaji nchini India na China ni za chini, hivyo, mashirika ya software ya nchi zilizoendelea barani Amerika na Ulaya zinakabidhi baadhi ya shughuli za software kwa mashirika ya nchi hizo. Kutokana na kupokea shughuli hizo kutoka kwa mashirika ya kigeni, Mashirika mengi katika sehemu ya software ya Dalian yamejifunza na kukusanya uzoefu mwingi na hatimaye yanaweza kusanifu software zenye hakimiliki ya kujitegemea na kuinua uwezo wa ushindani. Ofisa mkuu wa sehemu hiyo Bw. Zheng Shiyu alieleza:

"Kuna mifano mingi kama huo katika sehemu hiyo. Baadhi ya mashirika yalisanifu software za matumizi kwa mashirika ya kigeni, lakini baada ya wataalamu na wahandisi wetu kufahamu teknolojia za bidhaa hizo, kwenye msingi wa kulinda hakimiliki, mashirika hayo yanaendeleza teknolojia hizo na kuzitumia katika bidhaa zenye hakimiliki ya kujitegemea."

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-20