Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-21 14:23:00    
Utungaji wa Mswada wa Katiba Nchini Iraq Wakwama

cri

Wajumbe wa madhehebu ya Shiya katika kamati ya utungaji mswada wa katiba tarehe 20 walitangaza kuwa wataacha kazi ya kutunga mswada wa katiba kwa siku moja. Katika siku hiyo wajumbe wanne wa madhehebu ya Shiya walitangaza kujitoa kutoka kwenye kamati ya utungaji mswada wa katiba kwa muda. Imefahamika kuwa wajumbe wa madhehebu ya Shiya katika kamati hiyo watafanya mkutano katika tarehe 21 na kuamua kama wataendelea kushiriki kwenye kazi ya kuandaa mswada wa katiba.

Sababu ya wajumbe hao kutaka kujitoa kutoka kamati hiyo inatokana na tishio la usalama wao. Mwezi uliopita kamati hiyo ilikubali kuongezwa kwa wajumbe 15 wa madhehebu ya Shiya waongezeke kwa 15 na washauri 10. Hii ilikuwa sababu ya watu wenye silaha kuwalenga wao. Kiongozi wa tatu wa "al-Qaeda" Bw. Abu Musab al-Zarqawi kwa mara kadhaa alionya kuwa atawaadhibu wajumbe wa Waarabu wa madhehebu ya Shiya. Tarehe 19 wajumbe watatu wa madhehebu ya Shiya wa kamati hiyo waliuawa.

Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na hatari ya usalama, wajumbe wa madhehebu ya Shiya kutoshiriki au kujitoa kutoka kwenye kamati ya utungaji mswada wa katiba ni hali mbaya sana kwa mchakato wa utungaji mswada huo, na italeta wasiwasi kama kazi ya utungaji itamalizika katikati ya mwezi Agosti kama ilivyopangwa.

Lakini, kazi ya utungaji mswada wa katiba haiwezi kuwakosa wajumbe wa madhehebu ya Shiya. Waarabu wa madhehebu ya Shiya wanachukua 20% ya watu wote wa Iraq, na wengi wako katika mikoa minne ya kati na ya magharibi ya Iraq. Ushiriki wa wajumbe wa madhehebu ya Shiya katika kamati ya utungaji mswada wa katiba unahusiana moja kwa moja na hatima ya katiba. Kutokana na sheria ya muda nchini Iraq, mswada wa katiba utamalizika kabla ya tarehe 15 mwezi Agosti, na mswada huo ukishindwa kupitishwa katika mikoa mitatu kati ya mikoa 18 ya Iraq mswada huo utakuwa bure na kamati ya utungaji mswada wa sheria itavunjwa na wajumbe wa kamati hiyo watachaguliwa upya.

Pili, kazi ya kuandaa mswada wa katiba imekaribia kumalizika. Tarehe 19 rais wa Iraq alisema kuwa kama akiweza kuafikiana na wajumbe wa madhehebu ya Shiya, basi mswada ungeweza kumalizika mwishoni mwa Julai. Lakini wajumbe wa madhehebu ya Suni, madhehebu ya Shiya na wa Kurd wanahitilafiana katika masuala mengi. Chama cha Kidemokrasi cha Kurd kinachoongozwa na Mesud Barzani tarehe 19 kimetoa mapendekezo manane, moja kati ya mapendekezo hayo ni kuwa Iraq iwe nchi ya shirikisho, haki ya kujitawala kwa watu wa Kurd ipanuliwe na sehemu ya Kirkuk iingizwe katika sehemu ya kujitawala ya Kurd. Lakini wajumbe wa madhehebu ya Suni wanapinga pendekezo hilo, wakisema kuwa kama sehemu ya Wakurd ikijitawala, basi sehemu nyingine pia zijitawale, kama hivyo ndivyo, basi mfarakano wa taifa utatokea. Kuna habari zinasema kuwa wajumbe wa madhehebu ya Shiya wanataka katiba iwe kama kanuni za Kiislamu kuhusu hadhi ya wanawake kwenye ndoa, talaka na urithi. Masuala hayo yote yanahitaji pande tatu zishiriki na kujadili kwa pamoja.

Tatu, Kushiriki kwa wajumbe wa madhehebu ya Shiya katika mambo ya siasa kunaweza kuzuia shughuli za vikundi vyenye siasa vya madhehebu ya Shiya, ama sivyo vitaleta vurugu na hata kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya madhehebu ya Suni na Shiya.

Baada ya tukio la kuuawa kwa wajumbe watatu wa kamati ya utungaji mswada wa katiba wanasiasa wa madhehebu ya Suni na Shiya walilani mauaji hayo, na walisema tukio hilo halitaathiri nia ya madhehebu ya Suni kushiriki katika mambo ya siasa. Lakini jinsi hali mbaya inavyoendelea imeleta matata. Ushirikiano kati ya watu wa madhehebu ya Suni, Shiya na wa Kurd hauwezi kukosekana katika utungaji mswada wa katiba.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-21