Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-21 15:45:31    
Wanafunzi wengi wa nchi za nje wasome nchini China

cri

Wizara ya elimu ya China hivi karibuni imetangaza kuwa, mwaka jana wanafunzi kutoka nchi za nje wapatao zaidi ya laki 1.1 walikuja China kwa masomo, na idadi ya wanafunzi hao imeongezeka kwa 42 % kuliko mwaka 2003. Ofisa wa wizara ya elimu ya China alidokeza kuwa, serikali ya China itaendelea kuchukua hatua za kuwahamasisha wanafunzi kutoka nje wasome na kufanya kazi nchini China.

Serikali ya China inatenga fedha maalum na kufanya juhudi za kuanzisha na kukamilisha utaratibu wa usimamizi, na kuandaa wataalam wengi wanaoshughulikia elimu ya wanafunzi kutoka nje ili kuwavuta wanafunzi wa nchi za nje waje China kusoma. Wakati huo huo, maendeleo ya mambo ya kidiplomasia na mambo ya uchumi ya China pia yanawavutia sana wanafunzi wa nchi za nje waje China kwa masomo. Ofisa husika wa wizara ya elimu ya China Bibi Chen Yinghui alisema:

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya mambo ya kidiplomasia, uchumi hasa elimu ya China, nchi nyingi zaidi zimetambua elimu ya ngazi ya juu ya China, na wanafunzi wengi zaidi wamechagua kuja China kusoma China. Wakati huo huo, maendeleo ya kasi ya uchumi wa china yameongeza mvuto wa China duniani, pamoja na mvuto wa utamaduni wa jadi wa China, yote hayo yamedumisha ongezeko kubwa la kasi la wanafunzi kutoka nje wanaosoma nchini China.

Mwaka jana wanafunzi kutoka nchi za nje walitapakaa katika vyuo vikuu 420 vya China katika sehemu mbalimbali nchini na idara nyingi za elimu, ni 95 % ya wanafunzi hao wanatoa ada za masomo wao wenyewe. Masomo ya wanafunzi hao yanahusu lugha, utamaduni, uchumi, sheria, fizikia na uhandisi, kilimo na tiba.

Kijana kutoka Korea ya Kusini Ki Joon Kwon ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha usimamizi wa uchumi katika Chuo kikuu cha Beijing. Anaona kusoma nchini China ni chaguo lake moja lenye busara kabisa katika maisha yake. Kwani makampuni makubwa ya Korea ya kusini hasa makampuni ya fedha yanahitaji sana watu wanaoijua na kuielewa China, hata serikali ya Korea ya kusini inawafuatilia zaidi watu wanaoijua lugha ya kichina. Mwanafunzi aliyehitimu masomo kutoka chuo kikuu maarufu cha China atapata huduma nzuri zaidi nchini Korea ya kusini kuliko mwanafunzi aliyehitimu masomo kutoka chuo kikuu maarufu cha Seoul cha Korea ya kusini. Alisema:

Kutokana na sera nafuu za serikali na makampuni makubwa, hivi sasa wakorea kusini wanaosoma nchini China wamekuwa wengi zaidi na zaidi.

Ofisa wa wizara ya elimu ya China bibi Chen Yinghui anaona kuwa, wanafunzi kutoka nchi za nje kama kijana huyo wa Korea ya kusini si kama tu ni daraja la urafiki na ushirikiano kati ya China na nchi za nje, bali pia ni mali yenye thamani ya nchi yao na nchi walikosoma. Amedokeza kuwa, idara za elimu za China zimechukua hatua mbalimbali kwa kuvutia wanafunzi wengi zaidi kutoka nchi za nje kusoma nchini China. Hatua hizo ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa elimu ya wanafunzi hao na maandalizi wa walimu wanaofundisha wanafunzi hao, kukamilisha utaratibu wa bima ya matibabu ya wanafunzi hao na kuwapatia wanafunzi hao huduma nyingi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-21