Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Bw. Charles Clarke tarehe 20 alitangaza kwenye baraza la chini la bunge la Uingereza kuwa serikali ina mpango wa kuweka orodha ya watu wenye msimamo mkali duniani, ili kupambana na ugaidi. Kutokana na mpango huo, watu wanaohubiri kwa maneno makali, kutoa hotuba ya kuchochea ugaidi na kuweka tovuti za shughuli hizo watachukuliwa kama watu wasio na manufaa kwa maslahi ya jamii na kusajiliwa katika orodha hiyo. Serikali ya Uingereza ina haki ya kuwafukuza watu hao nchini Uingereza au kuwazuia kuingia nchini humo. Pamoja na mfululizo wa hatua za kupambana na ugaidi zilizochukuliwa na serikali ya Uingereza baada ya milipuko mikubwa ya tarehe 7 mwezi Julai iliyotokea nchini humo, wachambuzi wanaona kuwa hali mpya zimeonekana katika mkakati wa kupambana na ugaidi nchini Uingereza.
Kwanza, kusisitiza chanzo cha itikadi nyuma ya shughuli za ugaidi. Raia wengi wa Uingereza wanachukua serikali ya Blair kupeleka jeshi kushiriki kwenye vita vya Iraq kama ni chanzo cha milipuko ya tarehe 7 Julai, lakini waziri mkuu Tony Blair alisisitiza kuwa mambo hayo mawili hayana uhusiano na kuwaonya Waingereza wasipotoshwe na nadharia ya Waislam wenye msimamo mkali. Blair aliongoza ufuatiliaji wa watu kwenye itikadi. Tarehe 10 Tony Blair alikutana na viongozi wa Waislam na wawakilishi wa mashirikisho ya Waislam na kusisitiza kupambana na itikadi ovu, ili kuzuia itikadi hiyo isiwatie moyo vijana kuwaua watu na kujiua.
Pili, kuzuia mashambulizi kutoka nchini Uingereza. Ni tofauti na mashambulizi ya ugaidi yaliyotokea katika nchi nyingine, watuhumiwa waliothibitishwa na polisi kuhusu mlipuko huo wote ni Waingereza, ingawa wana asili ya Waislam, lakini hao wote ni vijana walioelimishwa nchini Uingereza, jambo hilo linaeleza kuwa makundi ya kigaidi ya kimataifa sio tu yamepeleka magaidi barani Ulaya, bali pia yamewaandaa vijana wawe warithi wao barani Ulaya. Tarehe 18, vyama vitatu vikubwa vya Uingereza vilifikia makubaliano kuhusu sheria mpya ya kupambana na ugaidi.
Tatu, kutafuta kuwasiliana na mashirikisho ya Waislam. Tarehe 19, Bw Tony Blair alikutana na viongozi wa waislam wa Uingereza na wakilishi wa mashirikisho ya Waislam, na kukisisitiza kuwa serikali ya Uingereza itapambana na uovu huo pamoja na mashirikisho hayo kwa njia sahihi. Mashirikisho hayo yalieleza kupiga moyo konde kuwaadhibu Waislam wenye msimamo mkali.
Mwisho, kufanya raundi mpya ya kimataifa ya mapambano dhidi ya ugaidi kwa kupitia ushirikiano wa kimataifa. Milipuko ya London ilitokea wakati mkutano wa wakuu wa kikundi cha nchi nane unapofanyika. Viongozi waliohudhuria mkutano huo walieleza mara moja msimamo wa kushutumu vikali ugaidi. Tarehe 20, Bw. Tony Blair alipendekeza kuitisha mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi. Kama mkutano huo utaweza kufanyika, Uingereza itakuwa kiongozi wa mapambano mapya ya kimataifa dhidi ya ugaidi.
Idhaa ya kiswahili 2005-07-21
|