Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-21 18:05:17    
Bush akubali kusaidia ushirikiano kati ya Marekani na India katika sekta ya nyuklia

cri

Baada ya kuandaliwa mapokezi ya ngazi ya juu ya rais Bush wa Marekani, waziri mkuu wa India Manmohan Singh tarehe 20 alirudi India na "matunda mengi". Alipokuwa ziaranu huko Washington, Marekani na India zilisaini makubaliano 11 kuhusu ushirikiano katika sekta za usalama, uchumi na nishati.

Kutokana na makubaliano yaliyosainiwa kati ya Marekani na India, India itaweza kupata nishati za nyuklia na vipuri vya kujenga zana za nyuklia kutoka kwa Marekani na nchi nyingine, lakini India inapaswa kupokea usimamizi na ukaguzi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, tena inapigwa marufuku kufanya tena majaribio ya silaha za nyuklia au kuhamishia kwenye nchi nyingine teknolojia za silaha za nyuklia. Makubaliano hayo hayakuitaka India iache kuzalisha uranium ya ngazi ya kisilaha inayoweza kutumiwa katika kutengeneza silaha za nyuklia.

Zamani kutokana na India kukataa kusaini "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia", Marekani siku zote inapiga marufuku kuipatia India teknolojia ya nyuklia. Lakini safari hii hali imekuwa tofauti. Rais Bush si kama tu alisaini makubaliano na waziri mkuu wa India Singh kuhusu ushirikiano wa matumizi ya kiraia wa nishati ya nyuklia, na pia ameaidi kulishawishi bunge la taifa lirekebishe sheria ili kuiwezesha Marekani iisaidie "kihalali" India katika kuendeleza nishati za nyuklia.

Wachambuzi wanaona kuwa, kuhusu suala la nyuklia, Marekani inachukua msimamo tofuati juu ya India na nchi nyingine, kusudi lake limeonekana dhahiri.

Kwanza, Marekani inatilia maanani hadhi ya kijiografia ya India na nguvu yake ya athari ya kimkakati kwenye bara dogo la Asia ya kusini. Washington imeona kuwa, India yenye nguvu kubwa inaweza kuisaidia kuimarisha na kupanua maslahi ya Marekani barani Asia, hasa inaweza kuisaidia kupambabna na athari ya kiuchumi na kisiasa ya China inayoongezeka siku hadi siku. Ndiyo maana mwanzoni India haikutaka kusaini "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia", ingawa Marekani iliwahi "kuhamaki" kwa muda, lakini hivi sasa imeanza kujenga mawasiliano barabara na India.

Pili, Marekani inataka kuivutia India kwa kuifanya Iran ikae katika hali ya upweke. Habari zilisema kuwa, India na Iran zimepanga mpango wa kutenga dola za kimarekani bilioni 4 kwa kujenga bomba moja kubwa la kupeleka mafuta, ili kukidhi kwa kiasi fulani mahitaji ya nishati ya India. Wachambuzi wanaona kuwa, kidhahiri, Marekani imeahidi kupenda kuisaidia India kuboresha hali ya usalama wa nishati na kuimarisha ushirikaino kwenye sekta ya nishati, ili kuihimiza New Delhi iache mpango wa kujenga bomba kubwa la mafuta kati ya nchi na nchi.

Hatua hiyo ya Bush inapingwa na wabunge wengi wa Marekani. Baadhi ya wabunge wanamlaani Bush wakisema kuwa hatua yake ni kwa ajili ya kufurahisha nchi moja na kukiuka na kuharibu kanuni za kimataifa kuhusu suala la silaha za nyuklia. Wabunge wengi walisema kuwa, kama Marekani imeiahidia India namna hii, basi Marekani itafuata vigezo gani wakati inaposhughulikia suala la nyuklia la Iran na la peninsula ya Korea? Marekani itakuwa na kisingizio gani kuzitilia shinikizo Iran na Korea ya kaskazini kuhusu suala la nyuklia?

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-21