Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-21 20:25:24    
Wayahudi walowezi wa Shanghai wapenda China

cri

Zaidi ya miaka 60 iliyopita, wakati wa-nazi wa Ujerumani walipowakandamiza na kuwaua kiwazimu wayahudi barani Ulaya, nchi nyingi zilikataa kuwapokea wakimbizi wayahudi, lakini watu wa Shanghai wenye moyo mema waliwapokea wayahudi zaidi ya elfu 30. Hivi sasa wengi kati ya wayahudi wakimbizi hao wamefariki dunia, hata vijana wa wakati huo wametiwa mvi kichwani. Ingawa miaka mingi imepita, lakini walipozungumzia maisha yao huko Shanghai, China, bado wana kumbukumbu nzuri.

Bwana Kurt Nissbaum na mke wake Inga Nissbaum wenye umri wa miaka zaidi ya 70 wanaishi katika kitongoji cha sehemu ya magharibi na kati ya Israel. Mwaka 1939 ili kuepuka mateso ya wa-nazi, Bw. Kurt alipokuwa na umri wa miaka 11 na Bi. Inga alipokuwa na umri wa miaka 6 kwa mbalimbali walitorokea Shanghai kutoka Austria na Ujerumani pamoja na wazazi wao. Walifunga ndoa mjini Shanghai na kurudi nchini Israel mwaka 1949. Mwandishi wetu wa habari alipowatembelea, Bi. Inga alisimulia hadithi yao ya kukimbilia Shanghai, alikumbuka kuwa, mwezi Novemba mwaka 1939, baba yake alifungwa katika kambi ya wafungwa wayahudi, sharti la baba yake kuachiwa huru lilikuwa familia yake yote iondoke Ujerumani. Wakati huo, nchi nyingi za Ulaya zilikataa kuwapokea wayahudi, hivyo walipaswa kuja Shanghai, China kwa kupanda meli. Anasema:

"Mama yangu alinichukua kwenda Berlin, tulitaka kumwokoa baba kutoka kambi ya kumfunga. Wakati huo hakuna nchi iliyokubali kutupokea, shirika moja lililowasaidia wayahudi kuondoka Ujerumani lilituambia kuwa, tuliweza kupanda meli kwenda Shanghai,China."

Wakati familia ya Inga ilipowasili Shanghai, jeshi la uvamizi la Japan bado halikukalia mji huo. Mwanzoni baba yake alitaka kuanzisha ofisi ya wakili ili kujipatia maisha mazuri, lakini baada ya muda mfupi tu, mizinga ya wavamizi wa Japan ilivunja ndoto yao, baba yake alipoteza kazi, maisha ya familia nzima yalitegemea tu mshahara mdogo wa mama yake. Hata hivyo, maisha ya Inga yalikuwa mazuri zaidi kuliko marafiki zake waliobaki barani Ulaya, yeye na ndugu zake walipata elimu nzuri, hivyo anaona kuwa, ni China iliyomwokoa yeye na familia yake.

Tofauti na nchi za Ulaya zenye desturi ya kuwapinga na kuwatenganisha wayahudi, wachina walioathiriwa na mawazo ya confusian siku zote walichukua msimamo wa kuwavumilia na kuwapokea wahamiaji kutoka nje. Takwimu zilionyesha kuwa, toka mwaka 1933 hadi mwaka 1941, mji wa Shanghai uliwapokea wakimbizi wayahudi zaidi ya elfu 30 kutoka nchi za Ulaya. Mtaa wa wayahudi wa Shanghai ulikuwa mtaa mkubwa kabisa wa wayahudi katika sehemu ya Asia ya mbali, wayahudi walianzisha ofisi yao yenyewe, kujenga ukumbi wa wayahudi, shule na hospitali, kuunda klabu za aina mbalimbali na chama cha wafanyabiashara, kuendesha majarida yao, na kuunda makundi ya kisiasa, hata kumiliki jeshi lao. Bi. Sara Ross ambaye ni myahudi kutoka Russia aliyewahi kuishi mjini Shanghai kwa miaka kumi alisifu sana kwa uvumilivu na moyo mema wa wachina. Anasema:

"Tulijifunza maadili mengi mazuri kutoka kwa wachina. Wachina wanawaheshimu wazee na kuwapenda watoto, wengi wanaonekana kuwa na adabu, hivyo tuliweza kuishi nchini China kwa uhuru."

Bi. Sara ana umri wa miaka 91 mwaka huu, familia yake mwaka 1916 ilihamia mjini Harbin, kaskazini mashariki mwa China kutoka sehemu ya Siberia, Russia. Baada ya Japan kuanzisha vita ya uvamizi dhidi ya China, mji wa Harbin ulikumbwa na vurugu ya kivita, uchumi wake ulififia siku hadi siku, hivyo Bi. Sara na mume wake walipaswa kuhamia Shanghai kutafuta nafasi za ajira.

Mwandishi wetu wa habari alipoingia nyumbani kwa Bi. Sara huko Jerusalem, aliona kama ameingia katika familia ya kijadi ya mchina ya miaka ya 30 ya karne iliyopita. Vitu vyote vya nyumbani kwake vinaonekana kama vinasimulia hadithi ya tajiri yake ya huko Shanghai na upendo wao kwa China.

Baadhi ya wayahudi hata walishiriki katika vita ya kupambana na wavamizi wa Japan, na kujenga urafiki mkubwa na watu wa China. Daktari Jacob Rosenfeld kutoka Austria mwaka 1939 alikimbilia Shanghai, baada ya miaka 2 alienda katika kituo cha kupambana na wavamizi wa Japan katika sehemu ya kaskazini mashariki ya China akijipamba kama askofu wa Ujerumani, na kujishirikisha katika vita dhidi ya uvamizi wa Japan iliyoongozwa na chama cha kikomunisti cha China. Alifariki dunia mwaka 1952 nchini Israel. Baada ya Israel na China kuanzisha uhusiano wa kibalozi mwaka 1992, kaburi la Rosenfeld lilikarabatiwa na shirikisho la urafiki kati ya Israel na China lililoundwa na wayahudi walowezi wa China. Maonesho kuhusu hadithi yake nchini China yaliyofanyika mwaka 1999 yaliwavutia watu zaidi ya laki 2.5. Mkuu wa shirikisho la urafiki kati ya Israel na China Bwana Tedy Kaufman anasema:

"Bw. Rosenfeld alikuwa onesho la uhusiano wa kirafiki kati ya China na Israel, wayahudi waliwahi kufanya mchango kwa ukombozi na uasisiwaji wa nchi ya China. Hivyo maisha yake yamekuwa na umuhimu mkubwa kwa watu wa taifa la China na taifa la wayahudi."

Idhaa ya Kiswahili  2005-07-21