Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-21 21:36:45    
Dar es Salaam- Tanzania yazindua mpango wa kitaifa kufunza wataalamu wa tiba ya ukimwi

cri

Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania tarehe 20 huko Dar es Salaam alizindua mpango wa kitaifa utakaowezesha kupata wataalamu wa tiba kwa ajili ya kuhudumia waathirika na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kote nchini.

Mpango huo unaitwa The Tanzania Benjamin William Mkapa National HIV/AIDS Fellows Program, na utatoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi, wachunguzi wa maabara na washauri ambao watasambazwa hadi vijijini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, rais Mkapa alisema kuwa chini ya mpango huo, Mkapa Fellows Program, watumishi wa afya 30 watafunzwa kila mwaka na kusambazwa hadi vijijini ili kutoa tiba, ushauri pamoja huduma zote zinazohitajika kwa wenye matatizo ya ukimwi.