Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-22 16:08:15    
Kweli Israel itatekeleza mpango wake wa upande mmoja kabla ya wakati?

cri

Kutokana na kuwa baadhi ya maofisa waandamizi wanataka mpango wa upande mmoja wa Israel utekelezwe kabla ya wakati, waziri mkuu wa Israel Bw. Sharon tarehe 21 alisema kuwa Israel haitatekeleza mpango wake wa upande mmoja kabla ya wakati uliopangwa.

Naibu waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert tarehe 21 kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema wapinzani wa mpango wa upande mmoja hivi karibuni walifanya maandamo makubwa, na maandamano hayo sio tu yalisumbua sana serikali tena yalivuruga maisha ya kawaida ya wananchi, kwa hiyo anaunga mkono kutekeleza mpango wa upande mmoja mapema kabla ya wakati uliopangwa. Mmoja wa maofisa waandamizi ambaye hakutaka kutaja jina lake pia alisema kuwa, utekelezaji wa upande mmoja kabla ya wakati uliopangwa hauhusiani na sheria, na maofisa wa serikali ya Israel watajadiliana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Rice ambaye yuko ziarani nchini Israel kuhusu suala hilo.

Lakini Bw.Sharon alisema hayo ni maoni yake binafsi, kuhusu wakati wa kutekeleza mpango huo wa upande mmoja amekwisha kuamua, yaani utaanza kutekelezwa katikati ya mwezi Agosti kuondoa makazi ya walowezi wa Kiyahudi kutoka sehemu ya Gaza.

Sababu ya Ehud Olmert kutaka mpango huo utekelezwe mapema ni kuwa wapinzani wa mpango huo walikuwa wanafanya maandamano mengi makubwa katika siku za karibuni, na wanatishia kuwa watakwenda sehemu ya Gaza ili kuzuia utekelezaji wa mpango huo. Kutokana na hali hiyo, Bw. Sharon alitangaza kuwa mtu yeyote hataruhusiwa kuharibu utekelezaji wa mpango huo. Ili kuzuia maandamano, serikali ya Israel ilituma polisi elfu 20 na kusimama kama ukuta kuwazuia waandamanaji ndani ya kijiji kimoja kusini mwa Israel. Hatua hiyo iliapata mafanikio fulani, kwani waandamanaji wengi wameacha nia ya kwenda sehemu ya Gaza.

Chini ya shinikizo kubwa la wapinzani wa upande mmoja na vilio vya maofisa waandamizi vya kutaka utekelezwe mapema, serikali inaendelea kushikilia uamuzi wake kutokana na mawazo ya pande mbalimbali. Kwanza polisi na idara zote husika za serikali hazijawa tayari vya kutosha, na ushirikiano kati ya Palestina na Israel katika kazi kuondoa makazi ya wayahudi haujakamilika, na kuondoka salama na mpangilio wa maisha ya walowezi wa Kiyahudi ni matatizo yanayotatanisha, kwa hiyo utekelezaji wa mpango wa upande mmoja haujapevuka.

Pili, kutekeleza mapema mpango huo pengine kutasababisha mgogoro mkali kati ya walowezi wa sehemu ya Gaza na serikali. Serikali ya Isrel iliwahi kupanga kuondoa makazi mwishoni mwa mwezi Julai, lakini wakati huo ndipo kipindi cha siku ya kukumbuka uharibifu wa hekalu, wananchi wafanya maombolezo kwa wiki tatu, kwa hiyo serikali ya Israel imeahirisha utekelezaji wa mpango wa upande mmoja mpaka katikati ya mwezi Agosti. Kama utekelezaji wake ukifanywa mapema katika kipindi cha maombolezo utaharibu hisia za imani ya dini za walowezi wa Kiyahudi na kupingwa na wananchi wote wa Israel.

Utekelezaji wa mpango wa upande mmoja una maana kubwa, na kazi ya kuondoa makazi ya walowezi wa Kiyahudi ni ya utatanisho na inahusika na pande mbalimbali, kwa hiyo serikali ya Israel ilikataa kutekeleza mpango wa upande mmoja kabla ya wakati baada ya kutafakari kwa makini.

Idhaa ya kiswahili 2005-07-22