Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-22 16:23:57    
Watoto wa Beijing wajifunza sayansi kwa furaha katika siku za likizo

cri

Maonesho ya pili ya sayansi na teknolojia kwa watoto tarehe 20 mwezi Julai yalifunguliwa mjini Beijing katika jumba la makumbusho la jeshi la watu wa China, kauli mbiu ya maonesho hayo ni "ujana, sayansi na teknolojia, afya na ustaarabu". Maonesho mengi kuhusu sayansi ya kawaida na majaribio ya kisayansi ya kuvutia yameweka mazingira mazuri kwa watoto waliokuwa likizoni kujifunza sayansi kwa furaha.

Imefahamika kuwa, maonesho ya sayansi na teknolojia kwa watoto yaliyoanza kufanyika mwaka 2004, ni shughuli kubwa ya maonesho ya sayansi na teknolojia kwa watoto mjini Beijing katika likizo ya majira ya joto. Maonesho hayo kwa mara ya kwanza yameonesha sanaa ya vyombo vya kisasa vya mawasiliano, ambapo wasanii kumi kadhaa kutoka nchi nane duniani wameonesha matokeo yao mapya na mwelekeo wa maendeleo wa sayansi na sanaa, tarakimu na uenezi, mtandao na upashanaji habari.

Katika sehemu ya maonesho ya wadudu wa mitambo, nzige wa Asia, Hercules beetle na wadudu wengine walifanya vitendo mbalimbali na kuonekana kama wadudu wa kweli chini ya udhibiti wa kompyuta. Katika sehemu ya maonyesho ya upashanaji bahari wa kitarakimu, wafanyakazi kutoka kwa kituo cha televisheni cha Beijing, kituo cha Redio cha Beijing, na gazeti la alfajiri la Beijing wameleta zana za kupiga picha za video na kunasa sauti na studio ndogo ya utangazaji wa moja kwa moja, watoto wanaweza kupiga picha za video akiwa kama "mpiga picha mdogo" na "mtangazaji mdogo" kwa kuelekezwa na wafanyakazi wa huko ili kusikia furaha ya kuhariri vipindi vya redio na televisheni. Katika sehemu ya maonesho la gazeti la alfajiri la Beijing, watoto wanaweza kujifunza namna ya kuhariri makala za magazeti.

Sehemu inayowavutia watoto wengi zaidi ni maisha ya watu wa kale, watoto wanaweza kutengeneza wenyewe vyombo vya udongo, kupata moto kwa kupekecha ubao, kusukuma toroli, ili kuhisi wenyewe maisha ya watu wa kale.

Maonesho hayo pia yameweka sehemu ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, zimeoneshwa kazi mpya zaidi ya 50 za uvumbuzi za kisayansi zilizobuniwa na watoto nje ya darasa la shule za msingi, sekondari, vyuo vikuu na makampuni ya mjini Beijing. Kazi hizo ni pamoja na kengele ya vipofu, chombo cha kutoa tahadhari ya wizi, na mfumo wa ufugaji usio na uchafuzi, kazi hizo zinaonesha werevu na uvumbuzi wa wataalamu wa siku zijazo wa mji mkuu katika eneo la sayansi na teknolojia.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-22