Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-25 18:46:37    
Hali halisi ya Suala la nyuklia la peninsula ya Korea

cri

China, Korea ya kaskazini, Marekani, Korea ya kusini, Russia na Japan zitafanya duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea kuanzia tarehe 26 hapa Beijing, China, ambapo zitafanya majadiliano tena kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea.

Suala hilo lilianzia karne ya 20. Katika miaka ya 60 na 70 ya karne ya 20, ili kutatua matatizo ya upungufu wa raslimali na hali wasiwasi ya utoaji wa nishani nchini humo, Korea ya kaskazini ikaanza kujenga kituo cha kuzalisha nishati ya nyuklia. Mwaka 1990, Marekani ilitoa ushahidi wake wa picha zilizopigwa kutoka kwenye satlaiti ikitilia mashaka kuwa Korea ya kaskazini imekuwa na majengo na zana za kufanya utafiti na kutengeneza silaha za nyuklia, ikajidai kuwa itafanya ukaguzi juu ya majengo na zana hizo. Lakini Korea ya kaskazini ilitoa taarifa mara kwa mara ikisema kuwa haina mpango na uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia, wakati huo huo ilikuwa ikiilaani Marekani kuweka silaha za nyuklia nchini Korea ya kusini na kutishia usalama wake.

    

Mwezi Mei mwaka 1992 hadi mwezi Februari mwaka 1993, Korea ya kaskazini ilipokea ukaguzi mara 6 kutoka kwa shirika la nishati ya atomiki duniani juu ya majengo na zana za nyuklia. Mwezi Oktoba mwaka 1994, huko Geneva, Korea ya kaskazini na Marekani zilisaini Makubaliano ya Korea ya kaskazini na Marekani kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea. Kutokana na makubaliano hayo, Korea ya kaskazini ilikubali kufunga mpango wake wa nyuklia, na jumuiya ya uendelezaji wa nishati ya peninsula ya Korea ikiongozwa na Marekani inabeba jukumu la kuijengea Korea ya kaskazini vituo viwili vya kuzalisha nishati ya nyuklia ili kutatua tatizo la ukosefu wa umeme nchini Korea ya kaskazini, na kabla ya kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo, jumuiya hiyo kila mwaka itoe mafuta mazito ya tani laki 5 kwa Korea ya kaskazini.

Lakini kutokana na sababu mbalimbali, ujenzi wa miradi ulianzishwa mwezi Agosti mwaka 2002. Na mwaka huo serikali ya Marekani ilianza kuziingatia upya sera yake juu ya Korea ya kaskazini baada ya rais Bush kuiweka Korea ya kaskazini kwenye safu ya "nchi za kiini cha vitendo viovu". Mwezi Oktoba mwaka huo, mjumbe maalum wa Marekani James Kelly baada ya kuitembelea Pyongyang, Korea ya kaskazini, alitangaza kuwa Korea ya kaskazini imekiri mpango wake wa kusukuma mbele mpango wa uendelezaji wa uranium nzito, ambapo suala la nyuklia la peninsula ya Korea likafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Lakini Korea ya kaskazini ilisema kuwa haikukiri hata kidogo kuwepo kwa mpango mzima wa uendelezaji wa uranium nchini humo. Mwezi Desemba mwaka 2002, jumuiya ya uendelezaji wa nishati ya peninsula ya Korea ikiongozwa na Marekani ilisimamisha kutoa mafuta mazito kwa Korea ya kaskazini kwa kisingizio kwamba Korea ya kaskazini ilikiuka Makubaliano kati yake na Marekani. Na Korea ya kaskazini ililaani Marekani kutoijengea vituo vya kuzalisha nishati ya nyuklia kabla ya mwaka 2003 kwa kufuata makubaliano, ilisema kuwa Marekani haikuzingatia kikweli kuboresha uhusiano na Korea ya kaskazini.

Tarehe 22 Desemba mwaka 2002, Korea ya kaskazini ilitangaza kuanzisha tena mpango wake wa nyuklia na kutumia tena majengo na zana zake za kuzalisha umeme kwa nishati za nyuklia, na tarehe 10 Januari mwaka 2003 ilitoa taarifa ikitangaza kujitoa kutoka kwenye "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia".

Ili kutatua kiamani mgogoro wa nyuklia wa peninsula ya Korea, China na pande mbalimbali za jumuiya ya kimataifa zilifanya juhudi kubwa. Mwezi Aprili mwaka 2003, China, Korea ya kaskazini na Marekani zilifanya mazungumzo hapa Beijing. Mwezi Agosti mwaka huo, chini ya uendeshaji wa China, duru la kwanza la mazungumzo ya pande 6 lilifanyika Beijing.

Tarehe 25 Februali mwaka 2004, duru la pili la mazungumzo ya pande 6 lilifanyika Beijing, mazungumzo hayo yalijadili masuala halisi na kubainisha hatua za usawazishaji.

Tarehe 23 hadi 26 Juni mwaka 2004 duru la tatu la mazungumzo ya pande 6 lilifanyika Beijing, ambapo pande husika zilikubali kikanuni yafanyike mazungumzo ya duru la 4 kabla ya mwezi Septemba mwaka huo hapa Beijing, lakini kutoaminiana kati ya Korea ya kaskazini na Marekani, duru la 4 la mazungumzo hayo liliahirishwa bila kikomo.

Zaidi ya mwaka mmoja umepita, Korea ya kaskazini na Marekani kila upande umechukua msimamo wenye unyumbufu, baada ya majadiliano kati ya pande mbalimbali, tarehe 9 usiku, Korea ya kaskazini ilitangaza kukubali kurudi tena kwenye mazungumzo ya pande 6.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-25