Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-25 22:17:24    
Amri ya polisi ya kuua bila kujali kitu kingine inawatia wasiwasi waingereza (kill on the spot with no other admittance)

cri

Tarehe 22 polisi wa Uingereza walipokuwa wakiwasaka watuhumiwa wanaohusika na mashambulizi ya kigaidi, walimwua kwa makosa raia mmoja wa Brazil, vyombo vya habari vya Uingereza vilidokeza kuwa polisi walitenda kitendo hiki baada ya kupata amri ya kuua waharifu bila kujali kitu kingine. Kutokana na amri hiyo, polisi wanaweza kuwafyatulia risasi watu wanaotuhumiwa kuwa na mabomu, tena kuwafyatulia risasi vichwani. Tukio hilo la kumwua mtu kwa makosa na habari kuhusu amri ya kuruhusu polisi kuua watuhumiwa vinawashangaza na kuwatia wasiwasi waingereza.

Tarehe 22 Jean Charles de Menezes, ambaye fundi wa umeme mwenye asili ya Brazil, aliingia kwenye kituo cha Stockwel cha subway kutoka nyumba moja ya makazi iliyokuwa ikisimamiwa na polisi, kwa kuwa alituhumiwa kuwa ni gaidi kutokana na mavazi na sura yake, aliandamwa na kutakiwa kusimama, baada ya kukataa amri hiyo alipigwa risasi 5 na polisi kichwani na kufa papo hapo. Taarifa iliyotolewa na polisi katika siku ya pili ilisema kuwa baada ya uchunguzi, Menezes alithibitishwa kuwa hakuwa na uhusiano na tukio la milipuko, kifo chake ni msiba na ni tukio linalosikitisha watu.

Baada ya kutokea tukio hilo, wizara ya mambo ya nje ya Brazil ilitoa taarifa haraka na kuonesha mshangao na mashaka kwa kuuawa kwa makosa kwa raia wa Brazil na kusema, "Menezes alijitolea muhanga kutokana na makosa ya kiwango cha chini". Habari zinasema kuwa Brazil itaendelea kuwasiliana na Uingereza kuhusu tukio hilo.

Katika hali ya kawaida polisi wa Uingereza wanapofanya doria huwa hawachukui silaha, safari hiyo si kama tu walikuwa na silaha bali walimwua abiria wa subway wakiwa karibu naye katika hali ya kuweko kundi la watu, jambo hilo linawashangaza sana watu. Magazeti ya Uingereza yalisema kuwa polisi walipata amri kuwa endapo mtu akituhumiwa kuwa na mabomu na kujaribu kuyalipua, polisi wanatakiwa kumfyatulia risasi kichwani mwake, lakini wasimpige risasi mwilini mwake, kwenye mikono na miguu yake, kwani mtuhumiwa huenda anaweka zana za kulipua mabomu katika sehemu hiyo. Meya wa London Bw. Ken Livingstone alisema waziwazi kuwa ili kukabiliana na mtuhumiwa anayelipua mabomu na kujiua, polisi hawana budi kutekeleza sera hizo. Polisi wataendelea kutekeleza amri hiyo juu ya watuhumiwa wa aina hiyo.

Milipuko iliyotokea mara kwa mara mjini London inaleta vitisho kwa watu, tukio la Menezes kuuawa kwa makosa na utekelezaji amri ya kuua watuhumiwa vinafanya watu wa Uingereza kukosa imani na polisi kuhusu usalama wao, sababu ya polisi kumshuku Menezes inafanya watu kuona kuwa ni kubambikiza makosa Menezes.

Mwanzoni polisi walipoeleza sababu ya kumfuatia Menezes kuwa sura yake inafana na mtu wa Asia ya kusini. Polisi kufuatilia watu wenye sura ya watu wa Asia ya kusini imesababisha malalamiko ya jumuiya za watu wa Asia ya kusini na jumuiya za waislamu, licha ya kulaumu sera hizo za kuua watu, wana wasiwasi kuwa tukio la kuuawa kwa Menezes kwa makosa ni mwanzo wa kuua watu wasio na makosa baada ya kutokea matukio ya milipuko ya London tarehe 21 mwezi Julai. Watu wenye asili ya nchi nyingine pia walieleza wasiwasi wao kuhusu "kuzingatiwa zaidi na polisi".

Vyombo vya habari vya huko vilitoa maelezo yakisema kuwa hivi sasa watu licha ya kuwa na tahadhari juu ya mashambulizi ya kigaidi, wanatakiwa kuepusha kuwaelewa vibaya na polisi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-25