Muungano wa nchi nne, Japan, Ujerumani Brazil na India, na Umoja wa Afrika tarehe 25 ulifanya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje huko London, pande hizo mbili hazikuafikiana katika suala la upanuzi wa Baraza la Usalama. Ingawa pande mbili zimekubaliana kuwa zitaendelea kufanya mazungumzo, lakini mpango wa kuwasilisha pendekezo la upanuzi wa Baraza la Usalama mwishoni mwa mwezi huu kama unavyotarajiwa na "muungano wa nchi nne" hautaweza kutimizwa, juhudi za "muungano wa nchi nne" za kujaribu kupata uungaji mkono kutoka Umoja wa Afrika zimekwama.
Pande zote mbili hazikudokeza habari baada ya mkutano kumalizika. Wachambuzi wanafafanua kuwa Umoja wa Afrika unashikilia msimamo wake wa awali ambao unakataa kurudisha pendekezo lake la upanuzi wa Baraza la Usalama. Katika hali hiyo muungano wa nchi nne hautapata kura za kutosha, kwa hiyo muungano huo unapaswa kuahirisha tarehe ya upigaji kura na katika muda huo utafanya juhudi za kushawishi Umoja wa Afrika.
"Muungano wa nchi nne" na Umoja wa Afrika kwa nyakati tofauti uliwasilisha mapendekezo yao kwenye Baraza la Usalama. "Muungano wa nchi nne" unataka kuongezwa nchi sita wajumbe wa kudumu na nchi nne zisizo wajumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama, na kutoa pendekezo la kuwa haki ya kupiga kura ya turufu kwa nchi wajumbe wa kudumu itajadiliwa baada ya miaka 15. Umoja wa Afrika unataka kuongezwa kwa nchi sita zenye haki ya kupiga kura turufu na nchi tano zisizo wajumbe wa kudumu. Tofauti kati ya pande mbili ni kuwa nchi zisizo wajumbe wa kudumu zinazidi kwa nchi moja kuliko pendekezo la muungno wa nchi nne, pili ni kuwa nchi wajumbe wa kudumu wanaotaka waongezwe wawe na haki ya kupiga kura ya turufu.
Katika tofauti hizo, muhimu ni haki ya kura ya turufu. Wajumbe wa Umoja wa Afrika wanasema kuwa pendekezo la Umoja wa Afrika ni matokeo ya mashauriano ya nchi za Afrika, kwa hiyo hautaacha msimamo wake. Wachambuzi wanaona kuwa tokea Umoja wa Mataifa uanzishwe, nchi za Afrika hazijawahi kupata nafasi ya kuwa wajumbe wa kudumu katika Baraza la Umoja wa mataifa, umoja huo unataka kugeuza hali hiyo wakati Umoja wa Mataifa unapofanya mageuzi. Lakini kuwa nchi mjumbe wa kudumu bila kuwa na haki ya kura ya turufu, nchi za Afrika zitakuwa hazina sauti katika maamuzi ya Baraza la Usalama, kwa hiyo Umoja huo unashikilia kwamba nchi wajumbe wa kudumu lazima ziwe na haki ya kura ya turufu. Hii inamaanisha kuwa nchi za Afrika zinataka uamuzi wa Umoja wa Mataifa ufanywe kwa demokrasia zaidi na kulaani nchi kubwa kutumika kiholela haki zao za kura ya turufu.
Kuwa na haki ya kura ya turufu pia ni matumaini ya "muungano wa nchi nne". Sababu ya kujadili haki hiyo baada ya miaka 15 ni kwa ajili ya kujipatia kura nyingi, lakini bila kutarajiwa ni kuwa Umoja wa Afrika pia umeingia katika upanuzi wa Baraza la Uslama, nchi ambazo muungano wa nchi nne unatamani zipate kura kutoka nchi za umoja huo sasa zimekuwa wapinzani. Katika mwezi huu pande mbili zilifanya mazungumzo mara nyingi, lakini kuhusu haki ya turufu hazikuafikiana.
Bila ya kura za nchi 53 za Umoja wa Afrika muungano wa nchi nne utapoteza theluthi mbili za kura. Kwa hiyo mjadala kati ya umoja wa Afrika na muungno wa nchi nne utakuwa mkali.
Kutokana na tofauti kati ya Umoja wa Afrika na Muungano wa Nchi Nne watu wamefahamu kuwa nchi za Afrika zimekuwa nguvu muhimu katika mambo ya siasa duniani, na muungano wa nchi nne ukitaka kuingia katika Baraza la Usalama hauwezi kukwepa kizingiti hicho cha Afrika.
Idhaa ya Kiswahili 2005-07-26
|