Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-27 16:33:23    
Pande zote sita za mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la penisula la Korea zaonesha msimamo wa unyumbufu na uaminifu

cri

Duru la nne la mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la penisula la Korea lilianza saa tatu asubuhi tarehe 26 katika Jumba la Wageni wa Taifa la Diaoyutai mjini Beijing. Ingawa mazungumzo yameanza punde tu na pande zote bado ziko katika kipindi cha kubadilishana maoni, lakini kutokana na hali ilivyokuwa katika siku ya kwanza, pande zote sita zimeonesha msimamo wa unyumbufu na uaminifu kuhusu utatuzi wa suala la nyuklia.

Msemaji wa ujumbe wa China Bw. Qin Gang kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jioni ya siku hiyo alisema kuwa kutokana na hali ilivyokuwa katika siku ya kwanza, pande zote sita zimeonesha msimamo wenye juhudi na makini. Pande zote zilibadilishana maoni kinaganaga zikiwa na matumaini mema kuhusu duru hili la mazungumzo, na zilisema kuwa zitathamini fursa hiyo kutafuta njia ya utatuzi wa suala la nyuklia la penisula la Korea kwa mazungumzo ya kutosha.

Wachambuzi wanaona kuwa unyumbufu na uaminifu wa pande sita unaonekana katika pande tatu zifuatazo: Kwanza, kutokana na hotuba za ufunguzi, kila upande ulisisitiza lengo la kutokuwa na nyuklia katika penisula la Korea, na kukubali kusukuma mchakato wa mazungumzo ya pande sita na kutatua suala la nyuklia kwa njia ya mazungumzo. Mkuu wa ujumbe wa Korea ya Kaskazini Bw. Kim Kye-gwan alisema, ujumbe wake uko tayari kufanya juhudi uwezavyo na kushirikiana na pande zote kupata akili za ufumbuzi. Mkuu wa ujumbe wa Marekani Bw. Christopher Hill alisema, Marekani inatambua Korea ya Kaskazini kuwa ni nchi yenye madaraka, na Marekani haina nia ya kuishambulia Korea ya Kaskazini. Kama Korea ya Kaskazini ikiacha nyuklia, Marekani itazingatia suala la usalama na nishati la Korea ya Kaskazini.

Pili, mazungumzo ya duru hili yatafanyika kwa aina nyingi, tofauti na mazungumzo ya duru la tatu, kwamba yatapangwa mazungumzo ya pande mbili mbili na mazungumzo ya pande mbalimbali kwa pamoja. Kabla ya duru hili kuanza, pande mbalimbali ziliwahi kufanya mazungumzo ya pande mbili mbili. Kwenye ufunguzi wa tarehe 26 pande mbalimbali zilikaa pamoja na zilionesha nia ya kusukuma mazungumzo yapate mafanikio na kutimiza lengo la kutokuwa na nyuklia katika penisula ya Korea, kisha wakuu wa ujumbe wa pande mbalimbali walikutana kwa dakika chache na kuanza mazungumzo ya pande mbili mbili.

Bw. Qin Gang alisema, sababu ya kuyafanya mazungumzo ya duru hili yawe ya aina tofauti ni kutaka kufanya mazungumzo ya pande mbili mbili kwa mara nyingi ili kupata makubaliano katika masuala fulani na kisha kujadili kwenye mazungumzo ya pande zote, Kufanya hivyo kunasaidia mazungumzo yapate mafanikio.

Tatu, ajenda ya mazungumzo inaweza kubadilishwa kwa mujibu wa hali itakavyokuwa ili pande zote zipate mjadala wa kutosha. Ajenda hiyo inayoweza kubadilishwa inaonekana katika mambo yafuatayo. Kwanza, duru hili la mazungumzo halikuwekwa muda maalumu ili mjadala uwe wa kutosha. Pili, ratiba ya mazungumzo inaweza kurekebishwa kwa mujibu wa hali itakavyokuwa. Inasemekana kwamba katika mazungumzo yafuatayo ya pande mbili mbili na ya pande zote yatarekebishwa kwa mujibu wa hali itakavyokuwa.

Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na kuwa hivi sasa misimamo ya pande mbalimbali bado inatofautiana, pengine mazungumzo yatakuwa magumu, lakini ilimradi tu pande zote zikijadiliana vya kutosha na kwa uvumilivu, mazungumzo hayo yatapata maendeleo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-27