Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-27 20:44:20    
Mapishi ya vipande vya nyama ya samaki kwa mchuzi wa nyanya

cri

Mahitaji

Samaki gramu 200, mchuzi wa nyanya gramu 50, vipande vya vitunguu saumu, vitunguu maji na tangawizi kila kimoja gramu 5, wanga gramu 15, M.S.G gramu 1, chumvi gramu 5, ute wa yai moja, mafuta ya ufuta gramu 1, mvinyo wa kupikia gramu 10, sukari gramu 10, mafuta gramu 500.

Njia

1. ondoa viungo vya ndani na mifupa ya samaki, kata nyama ya samaki iwe vipande vyenye urefu wa sm 2, viweke kwenye bakuli moja na tia mvinyo wa kupikia, ute wa yai, chumvi na wanga, kisha korogakoroga.

2. pasha moto tia mafuta ndani ya sufuria, mpaka yawe na joto la nyuzi 70, tia vipande vya nyama ya samaki kwenye mafuta na kuvikaanga mpaka viwe na rangi ya hudhurungi, kisha vipakue.

3. tia mafuta kidogo kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 50, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tagawizi, koroga koroga, tia mchuzi wa nyanya, sukari, mvinyo wa kupikia, M.S.G na maji kidogo, korogokoroga, mimina maji ya wanga, halafu mimina mafuta ya ufuta, washa moto, halafu imimina mvinyo wa kupikia kwenye vipande vya samaki. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.