Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-27 21:23:10    
Mbona nafasi ya kurusha ndege inayobeba satelliti ni ndogo sana

cri

Habari mpya kutoka idara ya usafari za anga ya juu ya Marekani zinasema kuwa urushaji wa ndege ya kubeba satelliti inayojulikana kwa "Discover" utaahirishwa kwa siku zaidi ya mbili. Uamuzi huo ulitangazwa katika saa mbili unusu kabla ya wakati uliopangwa wa kurusha ndege ya "Discover", hivyo unafuatiliwa na watu wengi.

Safari hiyo kuchelewa kurushwa kwa ndege ya "Discover" kulitokana na tatizo lililotokea katika chombo cha kuchunguzia hali ya nishati cha ndege hiyo. Chombo hicho kinafanya kazi ya kuzima ijin kuu wakati nishati inapokuwa chache kupita kiasi ili kuhakikisha usalama wa ndege, endapo katika wakati wa kurusha ndege hiyo kuwasha au kuzima kwa makosa kutasababisha ajali kubwa, hivyo kuchelewa kurusha ndege ya "Discover" kulienpusha ajali kubwa. Lakini hali hiyo pia inamaanisha kukosa nafasi moja nzuri ya kurusha ndege hiyo inayobeba satelliti.

Nafasi za kurusha ndege ya "Discover" ni kidogo sana ambayo ni mara mbili kwa siku zenye dakika 5 tu kila mara kutokana na upigaji hesabu wa maofisa wa elimu ya nguvu ya urukaji.

Nafasi hiyo ya urushaji inaamuliwa na mambo matatu ambayo ni la kwanza, "Discover" inapaswa kuwa katika mstari mmoja na mzunguko wa kituo cha kimataifa kilichoko katika anga ya juu. La pili, njia ya kupanda juu kwa ndege ya "Discover" lazima ni kuelekea upande wa kaskazini kuto upande wa kusini ili kuhakikisha kuwa ndege hiyo inaweza kutua kwenye uwanja maalumu nchini Marekani wakati wa dharura, hivyo nafasi ya mara mbili kwa siku ikabaki mara moja tu. Tatu, wakati wa kurusha ndege ya "Discover" unatakiwa ni katika mchana wa siku nzuri yenye jua ili kuhakikisha kuwa ndege zilizoko katika sehemu ya nje ya ndege zinafanya kazi barabara, hivyo hata nafasi ya mara moja kwa siku inaweza kukosekana.

Ndege inayobeba satelliti inavipuri milioni kadhaa hata kuzidi milioni kumi ambavyo vinafanya ndege kukabiliwa na hatari nyingi. Ili kuhakikisha usalama, ndege hiyo inatakiwa kukaguliwa kwa makini kabla ya kurushwa angani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-27