Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-28 15:47:02    
Mfereji Ling wenye historia ndefu

cri

Mfereji Ling wenye urefu wa kilomita 34 uko katika wilaya ya Xing'an ambayo iko umbali wa kilomita 66 kusini mashariki ya mji wa Guilin. Mfereji huo ulijengwa katika Enzi ya Qin (221k.k.-206k.k.) wakati Mfalme Qinshihuang aliposhika madaraka, na ni mfereji uliojengwa zamani zaidi nchini China na duniani. Mfereji huo uliwahi kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sehemu ya kusini ya China. Usanifu wa kisayansi, miundo mizuri na ufundi wa ujenzi wa mfereji huo hivi sasa bado ni mfano mzuri kwa ujenzi wa miradi ya maji.

Kati ya mabonde ya Mto Changjiang na Mto Zhujiang kuna milima mingi mikubwa, hivyo usafirishaji katika sehemu hiyo ni mbaya. Na usafirishaji kwa njia ya mito ni usafirishaji rahisi zaidi.

Mfereji Ling umetumika kwa zaidi ya miaka elfu mbili, bidhaa zinazozalishwa katika sehemu ya kaskazini na mazao yaliyozalishwa katika sehemu ya kusini yote yalisafirishwa kwenye mfereji huo. Hata katika miaka ya 30 hadi miaka ya 40 ya karne iliyopita, usafirishaji kwenye mfereji huo bado ulikuwa bado ni mkubwa.

zaidi ya miaka mbili iliyopitai, mafundi wa Enzi ya Qin walitumia utaalamu wao mkubwa na hata wengine walikufa wakati wa kuchimba mfereji huo.

Tunaweza kuona kuwa, njia ya kuchimba mfereji huo haikuwa fupi. Kwa nini mafundi wa Enzi ya Qin hawakuchimba mfereji mfupi zaidi? Sababu yake ni kuwa tofauti kati ya kina cha maji kwenye matawi ya Mto Xiangjiang na Mto Lijiang ni mita 7. Inamaanisha kuwa, ilikuwa ni lazima mafundi wajenge ukingo wenye urefu zaidi ya mita 7. Lakini kazi hiyo haikuweza kutimizwa katika Enzi ya Qin. Hivyo mafundi hao walichimba mfereji huo kwenye sehemu yenye mwinuko mkubwa zaidi kutoka usawa wa bahari, hivyo walihitaji kujenga ukingo wenye urefu wa mita 2 hadi 3 tu. Na kazi hiyo haikuwa mguvu sana katika Enzi ya Qin. Tena sehemu ya kaskazini ya mfereji huo inapindapinda, bila shaka mfereji huo ni mrefu zaidi kutokana na sababu hiyo, kwa nini mafundi walifanya hivyo?

Tofauti ya kina cha maji ni muhimu sana kwa Mfereji Ling. Ingawa kazi ya kuchimba mfereji ulionyooka ni rahisi zaidi, lakini kutokana na tofauti kubwa ya kina cha maji, itakuwa ni vigumu zaidi kuendesha mashua kwenye mfereji ulionyooka.

Ukingo mkubwa wa Tianping na ukingo mdogo wa Tianping ni sehemu mkubwa ya mradi wa Mfereji Ling, pia ni ajabu katika historia ya majengo ya maji nchini China. Umbo la ukingo wa Tianping si kama mstari unaonyooka, bali ni kama herufi ya V. Umbo hilo linaweza kupunguza shinikizo kubwa la maji. Mafundi wa Enzi ya Qin pia waliweka milingoti kwenye ukingo huo, ili kuimarisha msingi wa ukingo. Labda kutokana na sababu hizo, ukingo wa mfereji huo uliendelea kutumika kwa miaka zaidi ya elfu mbili..

Mradi huo mzuri unawastaajabisha sana watu. Pia kuna hadithi nyingi kuhusu mfereji huo wenye historia ndefu. Mababu waliochimba mfereji wa Ling walivinufaisha vizazi vya baadaye kwa busara zao.

Idhaa ya Kiswahili  2005-07-28