Baraza kuu la WTO tarehe 27 liliitisha mkutano tarehe 27 mjini Geneva. Mada kuu ya mkutano huo ni kujadili suala kuhusu mazungumzo ya raundi ya Doha na kujitahidi kuendeleza mazungumzo ya raundi ya Doha kabla ya likizo ya mwezi Agosti.
Mwezi Novemba mwaka 2001, mkutano wa nne wa mawaziri wa WTO uliofanyika mjini Doha, mji mkuu wa Qatar ulizindua mazungumzo ya raundi mpya ya biashara ya pande nyingi. Mazungumzo hayo yanayoitwa "raundi ya Doha" na kuthibitisha maeneno manane ya mazungumzo, yaani kuidhinisha mazao ya kilimo na yasiyo ya kilimo kuingia kwenye soko, huduma, haki miliki, kanuni, utatuzi wa migogoro, biashara na mazingira pamoja na biashara na maendeleo. Mazungumzo ya raundi ya Doha yamekwama kutokana na kutofikia makubaliano katika suala la kilimo.
Mkutano wa sita wa mawaziri wa WTO utafanyika mwishoni mwa mwaka huu huko Hong Kong. Wanachama 148 wa WTO wote wanatumai kuwa mkutano wa Hong Kong utafikia makubaliano ya kwanza kuhusu mazungumzo ya raundi ya Doha na kutumai kuwa utamaliza mazungumzo ya raundi hiyo kabla ya mwisho wa mwaka 2006. Sasa umebaki muda usiotimia miezi mitano kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa Hong Kong, lakini wanachama wa WTO bado hawajafikia makubaliano katika masuala muhimu ya mazungumzo ya raundi ya Doha.
Kikwazo kikubwa kabisa kinachozuia mazungumzo hayo ni suala la ruzuku ya kilimo. Nchi zinazoendelea zinataka Marekani na Umoja wa Ulaya ufute ruzuku ya mazao ya kilimo yanayouzwa katika nchi za nje, kupunguza ushuru wa forodha wa kilimo na kuleta mazingira sawa kwa mazao ya kilimo ya nchi zinazoendelea katika ushindani. Marekani na Umoja wa Ulaya uliahidi kwa mdomo kupunguza ruzuku ya kilimo, lakini ukweli ni kuwa ulalamikiana na kutazamana tu. Nchi zilizoendelea pia zinataka nchi zinazoendelea zifungue soko la huduma za benki na bima.
WTO tarehe 26 ilieleza kuwa mwezi uliopita, mazungumzo ya kilimo yakiwa suala muhimu la mazungumzo ya raundi ya Doha hayakupata maendeleo yoyote. Mkurugenzi mkuu wa WTO Bw. Supachai Panitchpakdi alieleza kuwa mazungumzo hayo ya raundi ya Doha yamekutana na matatizo na ana wasiwasi katika jambo hilo.
Mkutano huo wa baraza kuu la WTO umefanyika katika mazingira hayo. Mada muhimu ya mkutano huo ni kuidhinisha mazao ya kilimo na yasiyo ya kilimo kuingia sokoni, huduma na maendeleo. Mkutano huo utathibitisha masuala muhimu yatakayojadiliwa kabla ya mkutano wa Hong Kong, ili wanachama mbalimbali wa WTO wajitahidi kufanya matayarisho kwa ajili ya mkutano wa Hong Kong baada ya kumaliza likizo ya mwezi Agosti.
Idhaa ya Kiswahili 2005-07-27
|