Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-29 21:13:15    
Hali ya Mkoa wa Tibet

cri

Ufugaji ni njia muhimu ya uchumi mkoani Tibet, na una historia ndefu na una nafasi kubwa ya kuendelea zaidi. Hivi sasa kuna mbuga za majani zenye ukubwa karibu hekta milioni 82, kati ya eneo hilo mbuga zinazoweza kutumika kwa ajili ya malisho ni hekta milioni 56, kiasi ambacho moja kwa tano ya malisho yote nchini China na ni moja ya sehemu tano kubwa za ufugaji nchini China.

Ufugaji unachukua 60% ya uchumi wa Tibet, wanyama wanaofungwa ni nyati na kondoo. Wanyama hao ni wa kabila la Tibet, ambao wanasifa ya kuvumilia baridi na ukame.

Misitu

Mkoani Tibet kuna misitu yenye maeneo hekta milioni 6.3 ambayo ni 5% ya ardhi yote ya mkoa. Misitu hiyo ni akiba ya magogo yenye ujazo wa mita bilioni 1.4, ambayo inachukua nafasi ya pili nchini China. Miti mingi katika misitu hiyo ni misonobari ambayo ina sifa ya kukua haraka.

Mkoa wa Tibet unatilia maanani sana hifadhi ya mazingira. Sehemu 18 za hifadhi mazingira zimeanzishwa ambazo ni asilimia 33.9 ya ardhi yote ya Tibet.

Mradi wa Kuusaidia Mkoa Tibet

Mkoa Tibet ambao unajulikana kama ni paa la dunia uko nyuma kiuchumi kutokana na sababu za kihistoria na mazingira ya kimaumbile. Mwaka 1994 serikali kuu ilifanya mazungumzo ya mara ya tatu na inaanzisha mradi wa kuusaidia Mkoa Tibet, mradi huo unahusu, ufugaji, misitu, nishati, mawasiliano, mawasiliano ya posta, jumla unahitaji yuan bilioni 4.86. hivi sasa mradi huo umekamilika na kuanza kutoa mchango mkubwa.

Msaada wa Mkoa Tibet umesaidia kuboresha maisha ya watu wa Tibet. Mjini Lhasa wenyeji wanaweza kuangalia TV, majumba ya ghorofa yamejengwa badala ya zile nyumba za chini za zamani, watoto wa wakulima wanaokwenda shule, bendera za rangi mbalimbali zinapepea mbele ya Kasri la Potala zikiwavutia watalii kwa mwaka mzima.

Maliasili ya Utalii Mkoani Tibet

Maziwa

Mkoani Tibet kuna maziwa zaidi ya 1500 yenye eneo la kilomita za mraba 240 ambayo ni theluthi moja ya eneo lote la maziwa kote nchini China. Maziwa ya mkoani Tibet sio tu yana maeneo makubwa bali pia yana vina virefu.

Maziwa kwa lugha ya Kitibet ni "namucuo", maana yake ni maziwa mbinguni. Kwa kweli maziwa hayo chini ya mbingu ya buluu yanaonekana kama vioo hapa na pale vikiwa pamoja na mbuga za majani na yanaleta mandhari nzuri sana katika paa la dunia.

Kasri la Potala

Kasri la Potala liko mlimani kaskazini magharibi mwa mji wa Lhasa, ni kasri lililo juu kabisa duniani. Kasri hilo lilijengwa katika karne ya 7, lina ghorofa 13 na eneo la hekta 41. kasri hilo limepakwa rangi ya dhahabu na kutiwa lulu zaidi ya 4000, ni mahali pa dini ya Buddha anapoishi, kufanya kazi na shughuli za kidini.

Mwaka 1961 kasri la Potala iliorodheshwa katika orodha ya urithi wa kitaifa, kila mwaka serikali kuu inatenga fedha kwa ajili ya ukarabati wake. Tokea mwaka 1989 hadi 1994 serikali kuu ilitenga yuan milioni 5.3 kwa ajili ya ukarabati wake.

Hekalu la Dazhao

Hekalu la Dazhao lililoko katikati ya mji wa Lhasa lilijengwa mwaka 647, lilijengwa kwa ajili ya kumkaribisha binti wa mfalme wa Enzi ya Tang, Wen Cheng kuolewa na mfalme wa Tibet. Hekalu hilo limechanganya mtindo wa Nepal na wa Kichina.

Hekalu la Zhashlumbu

Hekalu la Zhashlumbu ni hekalu kubwa la dini ya Buddha mkoani Tibet, lina historia miaka 500, ni kituo cha kufanya shughuli za kidini.

Hekalu hilo lilijengwa kwenye mteremko wa mlima, lina kumbi zaidi ya 50 na nyumba zaidi 200. Ukumbi wa kuwekea sanamu ya Buddha una kimo cha mita 30, sanamu hiyo ilitengenezwa kwa dhahabu na shaba nyeusi, na ilitiwa almasi na lulu zaidi ya 1400.