Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-29 21:18:58    
Elimu ya Tibet

cri

Hali ya jumla ya elimu ya Tibet

China inatekeleza sera ya kutoa elimu bure mkoani Tibet. Gharama za masomo ya wanafunzi toka shule za msingi hadi vyuo vikuu zote zinatolewa na serikali. Sera hiyo nafuu inatekelezwa mkoani Tibet tu. Katika Tibet ya zamani, hakuna shule moja inayomaanisha hali ya zamani tulizo nazo, sembuse chuo kikuu, lakini hivi sasa kuna vyuo vikuu vinne mkoani Tibet.

Ili kusaidia Tibet kuendeleza elimu, tokea mwaka 1985, serikali kuu ya China ilianzisha daraja au shule ya Tibet katika mikoa na miji 21 nchini humo, ambapo wanafunzi elfu 10 hivi wa Tibet wamehitimu kutoka vyuo vikuu au shule za sekondari, na serikali kuu iliwalipia gharama zote za masomo.

Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2003, shule za ngazi na aina mbalimbali zipatazo 1011 zilijengwa mkoani Tibet, wanafunzi walifika laki 4.534, na asilimia 91.8 ya watoto wenye umri wa kwenda shule wamesoma shule; watu wasiojua kusoma au kuandika wamepungua na kufikia chini ya asilimia 30. Na tokea mwaka 1992, "shule za matumaini" zaidi ya 180 zilijengwa mkoani Tibet ili kunasaidia watoto wa familia zenye matatizo ya kiuchumi waende shule, ambapo wanafunzi elfu 36 walipata misaada.

Dini mkoani Tibet

Dini ya kibudha ya kitibet na mahekalu ya wa-lama

Dini ya kibudha ya kitibet imeenea kwenye sehemu ya Tibet na Mongolia ya ndani nchini China, wenyeji wa huko waliita dini hiyo kuwa ni "dini ya lama", hii ni dini ya kibudha iliyoenea Tibet kutoka India na sehemu za ndani za China ambayo iliunganishwa na dini za kale za huko na kuwa dini yenye umaalum wa kitibet.

Kutokana na athari ya dini ya kibudha ya kabla ya wahan la China na dini ya kibudha ya India, mahekalu ya dini ya kibudha ya kitibet mengi yalijengwa kwa mtindo wa jengo la kifalme la kabila la wahan tena kuonesha mtindo wa kitibet, kwa kawaida, mahekalu hayo ni makubwa sana yenye taadhima, mapaa ya majengo huchongwa nakshi na kuchorwa picha ambayo yanaonekana ya kupendeza sana. Kwa mfano, Kasri la Budara la Lahsa, Hekalu la Drepung na Hekalu ya Tar la Qinghai yote ni majengo mazuri ya zama za kale.

Ujenzi wa mahekalu ya Tibet pia hutilia maanani zaidi kwa kuonesha taswira, ajabu na miujiza ya dini ya kibudha ya kitibet. Mahekalu ya kawaida huwa na ukumbi mkubwa na mrefu wa kuabubu sanamu za budhaa, ndani kupambwa na mapazia ya kidini ya rangi mbalimbali, nguzo za ukumbini hupambwa kwa mazulia za rangi, ndani kuna giza kidogo, hivyo watu wakiingia huko hujisikia ajabu ya dini.

Desturi za kidini za Raia wa Tibet

Watu wa Tibet wana uelewa wa kutosha wa kuamini dini. Watu wengi wa makabila ya watibet, wabenba, waloba na wanaxi wa mkoa unaojiendesha wa Tibet ni waumini wa dini ya kibudha ya kitibet, pia kuna waumini wengi wa dini ya kiislamu na kikatoliki. Hivi sasa mkoani Tibet kuna sehemu zaidi ya 1700 za kufanyika shughuli za dini ya kibudha ya kitibet, watawa wa kiume na kike wanaokaa katika mahekalu wamefikia elfu 46; kuna misikiti minne, waumini wa dini ya kiislamu zaidi ya 3000; kanisa moja ya kikatoliki, waumini zaidi ya 700.

Watu wa kabila la watibet na makabila mengine madogo madogo mkoani Tibet wana haki na uhuru wa kuishi maisha na kufanya shughuli za jamii kwa kufuata desturi na mila zao wenyewe. Wanapodumisha desturi na mila yao ya jadi katika mavazi, chakula na makazi ya makabila yao, pia wamejifunza desturi mpya zinazoonesha ustaarabu wa zama za hivi sasa na maisha mazuri katika malazi na chakula pamoja na shughuli za kufunga ndoa au mazishi. Watu wa mkoa wa Tibet wanaendelea kufanya shughuli nyingi za jadi kama vile za kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa Tibet, sikukuu ya mavuno na sikukuu ya Xuedun pamoja na shughuli nyingi za kidini. Pia watibet wa hivi sasa pia wanafanya shughuli mpya za aina mbalimbali za China na ng'ambo.

Utamaduni wa Tibet

Tangka: Tangka ni tamshi la kitibet, nayo ni picha za rangi zilizotariziwa au kuchorwa kwenye vitambaa, hariri au karatasi. Picha hizo ni aina moja yenye mtindo wa utamaduni wa kabla la watibet.

Inasemekana kuwa, katika zama za kale, binti mfalme Wencheng alipoolewa Tibet, alikwenda na ufundi wa kufuma nguo, kutokana na picha hizo tunaweza kuona kuwa ufundi huo wa uzalishaji ulitumiwa na kuenea huko Tibet wakati huo. Rangi zilizotumika katika uchoraji wa picha hizo zilitengenezwa kwa njia ya kisayansi, ndani yake zilitiwa madini na mimea, tena hali ya hewa ya uwanda wa juu wa Tibet ni isiyo na unyevu, hivyo picha za Tangka hata zilichorwa karne kadhaa zilizopita, rangi zake bado zinaonekana ni nzuri za kupendeza kama zilivyo za picha mpya.

Yaliyochorwa kwenye Tangka yanahusu mambo yote ya maisha ya jamii, hata kama ni histoira ya jamii, na shughuli za kidini zimeoneshwa zaidi katika picha za Tangka.

Maua ya siagi

Maua ya siagi ni sanaa ya sanamu za mafuta. Sanaa hiyo inaonesha mambo mengi mbalimbali kuhusu hadithi za dini ya kibudha, hadithi ya Budha mkuu Sakyamuni, hadithi za historia, hadithi za opera. Sanamu za maua ya siagi ni za aina mbalimbali kama vile jua, mwezi, nyota na sayari, maua, miti, ndege , wanyama, vibanda na majumba na sanamu mbalimbali za mabuddha na mababu, Majemedari na watu mashuhuri. Sanamu hizo zilichongwa vizuri na kuonesha sura halisi ya kupendeza, ambazo ni vitu vya sanaa vya kiwango cha juu.

Sanamu ndogo ndogo za maua ya siagi zilizochongwa vizuri na kupakwa rangi ya kupendeza huchukuliwa kama sadaka za kutambika, aina zake mbalimbali zinaonekana ishara ya heri na baraka. Na sanamu nyingine za maua ya siagi huwekwa kwa pamoja ambazo zinawavuta watu kwa mitindo yao ya kufurahisha.

Opera ya kitibet

Opera ya kitibet ina historia ndefu tangu enzi na dahari, mitindo ya opera hiyo ni ya aina mbalimbali. Michezo ya Opera ya kitibet kama vile "Binti wa mfalme Wencheng" na "Mwana wa Mfalme Nosang" imekuwa michezo inayosifiwa na kupendwa na watu kwa miaka mingi tangu zamani, muziki wa michezo hiyo ni mwororo sana, vifuniko vya nyuso na mapambo ya nguo ya wahusika wa michezo hiyo ni ya rangi mbalimbali na kupendeza kiajabu. Yote hayo yameonesha msingi imara wa utamaduni kwenye opera ya kitibet.

Opera ya kitibet ni michezo ya sanaa inayoonesha nyimbo na ngoma za kienyeji. Toka karne ya 15, mtawa Tangdongjiebu wa madhehebu ya Geju alitunga michezo ya opera ya kitibet na kuongoza wachezaji kuonesha michezo ya nyimbo na ngoma iliyoeleza hadithi fupi katika sehemu mbalimbali. Baada ya miaka mingi, michezo ya opera ya kitibet imeendelea vizuri, michezo yenyewe ilitungwa kikamilifu na kusimulia hadithi nzuri na kuongeza vivutio mbalimbali pamoja na mapambo, mitindo tofauti ya uimbaji kwa kufuata bendi na uimbaji wa wanaoambatana, opera ya kitibet kweli ni michezo mbalimbali ya sanaa.

Watibet wanapenda sana michezo ya opera ya kitibet, kila yanapofanyika maonesho ya michezo ya opera hiyo, watu wengi kutoka sehemu za mbali hata wanaweza kumiminikia kwenye uwanja mmoja kutazama maonesho.

picha husika>>

1  2