Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-01 14:40:36    
Suala la nyuklia ya Iran lafuatiliwa tena

cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Hamid-reza Asefi tarehe 31 mjini Teheran aliuhimiza Umoja wa Ulaya utoe mapendekezo ya kutatua suala la nyuklia ya Iran kabla ya tarehe mosi, ama sivyo, Iran itaanzisha tena shughuli za mabadiliko ya uranium katika kipindi cha maandalizi ya shughuli za uranium nzito. Lakini Umoja wa Ulaya haukujibu msimamo huo wa Iran kwa haraka. Baada ya miezi miwili, suala la nyuklia ya Iran limefuatiliwa tena.

Msemaji Asefi alieleza siku hiyo kuwa Iran haitakubali kitendo cha Umoja wa Ulaya kuahirisha suala hilo. Kama matakwa ya Iran hayataridhishwa, Iran itaanzisha tena mara moja zana za kusafisha uranium zilizoko mjini Isfahan, katikati ya Iran. Lakini alisisitiza kuwa Iran bado inapenda kuendelea na mazungumzo na Umoja wa Ulaya na kusimamisha shughuli za uranium nzito.

Upande wa Iran ulidokeza kuwa nchi tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinazouwakilisha Umoja wa Ulaya kufanya mazungumzo na Iran, tarehe 30 zilitaka kuahirishwa kwa wakati wa kutoa mapendekezo ya kutatua suala la nyuklia la Iran hadi tarehe 7 mwezi Agosti, lakini Iran imepinga na pia imetumai kuwa mapendekezo hayo yatakidhi matakwa ya chini kabisa ya Iran. Rais Mohamed Khatami alieleza tarehe 27 kuwa, Iran inatumai Umoja wa Ulaya utairuhusu Iran iendelee kushughulikia uranium nzito, lakini haijali namna gani mapendekezo hayo yatakavyokuwa, Iran itaanzisha tena zana za kusafisha uranium. Vyombo vya habari vimeeleza kuwa Iran iko tayari kufanya mazungumzo ya nyuklia ya raundi mpya na Umoja wa Ulaya. Dalili mbalimbali zinaonesha kuwa Iran haitarudi nyuma na kushikilia msimamo wake kuwa Iran ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa amani.

Katika miezi miwili iliyopita, Iran ilimchagua rais mpya anayechulikuwa na vyombo vya habari vya magharibi kama mmoja wa kundi la wahafidhina, na Umoja wa Ulaya unafikiri kurekebisha mbinu za kufanya mazungumzo ya nyuklia. Lakini vyombo vya habari vya Ulaya vinaona kuwa, katika kanuni kubwa ya msimamo wa Umoja wa Ulaya kutatua suala hilo kwa mazungumzo, Umoja wa Ulaya hautabadilisha msimamo wake. Rais Chirac wa Ufaransa hivi karibuni alisisitiza matumaini yake kuwa, mazungumzo hayo yataweza kuondoa hatari ya kuenea kwa silaha za nyuklia kwa Iran.

Lakini msimamo wa Iran umeleta taabu kwa Umoja wa Ulaya kuamua vitendo vyake. Vyombo vya habari vya Ulaya viliona kuwa toka mwanzo, Iran ilishikilia msimamo wa kudumisha haki yake ya kutumia kiamani nishati ya nyuklia katika mazungumzo ya suala la nyuklia la Iran, na msimamo huo haujabadikilika hadi sasa, lakini ni vigumu kwa nchi za magharibi kukubali msimamo huo. Kutokana na hali hiyo, njia ya kutatua kabisa suala la nyuklia la Iran bado ni ngumu yenye taabu kubwa.

Idhaa ya kiswahili 2005-08-01